Kipindi cha Covid-19 watu wengi hawakupenda kuhudhuria sehemu zenye mikusanyiko na wengine walitumia muda mwingi kubaki nyumbani. Hii ilipelekea biashara nyingi  kuanguka na hali ya kiuchumi ya  wafanyabiashara wengi ilidhoofu.

Benki kuu ya Tanzania ilichukua hatua ya kupunguza riba ya mkopo katika mabenki ili kuwasaidia wafanyabiashara ambao wamesajiri biashara zao na wanaolipa kodi waweze kusimama tena kiuchumi.  
Lakini punguzo hili la riba halikuwahususisha watu ambao hawajasajiri biashara zao. Wasichana wengi wadogo ambao walikuwa wakimiliki biashara ambazo hazijasajiliwa walijikuta wanafunga biashara, wengine waliuza bidhaa zao zote kwa bei ya chini na ya hasara kwasababu ya kulipa madeni na kuweza kupata mahitaji muhimu ya chakula. 

Asilimia 89% ya wasichana wadogo  wafanyabiashara chini ya miaka 30 waliishia kupata anguko la kiuchumi. Kwa mujibu wa takwimu za TGNP kati wasichana 10 wanaotegemea wenza wao kifedha wasichana 5 wanapitia ukatili wa kijinsia na hawawezi kuondoka katika hayo mahusiano kwasababu  wanawategemea kifedha  wanyanyasaji.
kwa ufadhili wa Urgent Agency Africa Fund, shirika la Her Initiative ambalo limejikita katika kupunguza umaskini kwa wasichana na kuwatengenezea msingi imara wa kujitegemea kiuchumi liliamua kuandaa mafunzo kwa wasichana wadogo wafanyabiashara ambao bado hawajasajili rasmi biashara zao kupitia mradi wa songambele.

Shirika liliamini hatakama wamepitia mateso na shida bado wanayo nafasi ya kupiga tena hatua kama tu watapewa nafasi nyingine ya kufahamu umuhimu wa kusajili biashara zao pamoja na kulipa kodi.
Wasichana Mia moja kutoka Kinondoni, Ilala, Temeke, Kigamboni Na Ubungo walinufaika na mradi huu wa songambele. 

"Tumeamua kuandaa mafunzo haya ili wasichana wadogo wafanyabiashara waweze kuwa na biashara zenye ushindani kwenye soko, na ili waweze kufikia hii hatua  ni lazima kwanza warasimishe biashara zao." Zainabu Hassan Ally ( Finance and Logistic Officer) kutoka Her Initiative. 
"Usiposajili biashara yako kwa wakati utakuta jina lako tayari wengine wameshasajili." Mr Gabriel Girangei mwandamizi wa usajili kutoka Brela Tanzania. 

"Raha ya kulipa kodi, unakuwa huru na biashara yako, sio kukimbia kila siku kila ukiwaona wafanyakazi wa TRA, lakini nzuri zaidi unaongeza uaminifu kwa wateja wako." Mercy C Macha kutoka TRA Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...