Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MSIMAMIZI
wa uchaguzi wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi
amewataka wananchi waliojiandikisha kupiga kura kusikiliza Sera za
wagombea wanaojinadi hivi sasa na kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Myenzi
akizungumza jana amesema wananchi hao wanapaswa kujitokeza kwa wingi
ili wakapige kura siku ya jumatano ya Octoba 28 mwaka huu ili kuwachagua
wagombea wanaowapenda wao.
Amesema
hivi sasa wagombea wengi wanazungumza sera zao kupitia ilani za
uchaguzi hivyo wananchi wajitokeze kwenye mikutano ya hadhara ili
kuwasikiliza.
"Siku ya
kupiga kura mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwachagua wagombea
mnaowataka ninyi wenyewe katika ngazi ya urais, ubunge na madiwani,"
amesema Myenzi.
Hata
hivyo, amewataka wananchi wa Simanjiro kuchuja ahadi za wagombea ili
kutowachagua wale ambao wanawaahidi mambo ambayo hawawezi kuyatekeleza.
Amesema
wao kama wasimamizi wa uchaguzi wa eneo hilo wamejipanga kikamilifu
kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika bila vikwazo vyovyote.
Mkazi
wa kata ya Endiamtu, Sokota Mbuya amesema kampeni za uchaguzi mkuu wa
mwaka huu zimeanza na wagombea wa nafasi mbalimbali wameanza kujitokeza
kumwaga sera zao.
"Hivi
sasa wananchi wana uelewa wa kutosha tofauti na awali hivyo watawachagua
wagombea ambao watafanikisha maendeleo na siyo maneno matupu," amesema
Mbuya.
Mkazi wa kata ya
Mirerani Adam Woiso amesema wananchi wanapaswa kuchuja sera za wagombea
kupitia ilani ili wafanye uamuzi sahihi wa kupiga kura siku
itakapofika.
Woiso
amesema anatambua kuwa wananchi wa Mirerani hawatafanya makosa kwa
kuwachagua viongozi ambao hawajaacha alama ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akizungumza na wananchi wa Kata
ya Terrat.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...