Hayo yamewekwa wazi na Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine wakati alipotembelea na kufanya mazungumzo na uongozi wa NFCS-LTD kinachojihusisha na ununuzi wa Kahawa kwa wakulima wadogo wilayani Ngara mkoani Kagera.
Bw. Justine amefanya kikao na viongozi wa chama hiki cha ushirika ambao wamepata kueleza changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji ikiwa ni pamoja na kutokuwa na vyombo vya usafiri vitakavyowezesha wao kuwafikia wakulima wao na wakulima kukosa elimu ya kutosha kwenye zao la kahawa hivyo kufanya uzalishaji kuwa mdogo ikilinanishwa na uhitaji wa soko.
Bw. Justine amesema kuwa TADB ipo tayari kuleta wataalamu watakaosaidia kutoa elimu ya uoteshaji wa miche ya mikahawa mipya ili kuongeza kiwango cha uzalishaji.
Katika kikao hicho, Bw. Justine ameahidi kutoa pikipiki mbili (2) zitakazotumiwa na viongozi wa chama hicho kuwafikia wakulima wao kirahisi.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993, NFCS-LTD ilisitisha shughuli zake mwaka 2012 kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha na madeni yaliyokithiri.
Mwaka 2018 TADB ilifanikiwa kufufua chama hiki kwa kukitengenezea mfumo mzuri wa uendeshaji na kukipatia mkopo wenye riba nafuu na kukifanya kuwa na uwezo wa kukusanya kahawa yenye kufikia tani 2,300 kutoka kwa wakulima wadogo zaidi ya 500 walioko wilayani Ngara.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...