Na Mwandishi wetu, Babati
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, inamshikilia
mtumishi wa Baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Babati Ruth Reniel
Semkuyu kwa kosa la kudaiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki
moja kwa mkazi wa mkoa huo ili kukaza hukumu.
Mkuu
wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza mjini
Babati Septemba 9 amesema Semkuyu anadaiwa kutenda kosa hilo kwenye
ofisi ya ardhi.
Makungu
amesema Semkuyu alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 15 cha sheria
ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Amesema
awali walipata taarifa kutoka kwa mlalamikaji (jina lihahifadhiwa)
ambaye alishinda kesi yake katika moja ya mabaraza ya ardhi ya kata
hivyo alifika baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Babati ili kukaza
hukumu.
Amesema
alipofika alielezwa amuone Semkuyu ili ampe utaratibu wa kukaza hukumu
ambapo Semkuyu alimtaka kutoa shilingi 118,000 kwa madai kuwa ni gharama
ya kukaza hukumu.
"Mwananchi
huyu alitilia mashaka kiwango hicho hivyo akafika TAKUKURU na kuelezea
malalamiko yake nasi tukabaini kiwango kinachopaswa kutolewa kwa kukaza
hukumu ni shilingi 18,000 tuu," amesema Makungu.
Amesema
walimpa mwananchi huyo shilingi 118,000 na kisha akampelekea Semkuyu
ambaye alimpa shilingi 18,000 kwa ajili ya kuzilipia benki kisha arudi
na risiti ya malipo huku akibaki na shilingi laki moja.
"Baada
ya kukabidhiwa fedha hizo makachero wetu walimkuta na shilingi 100,000
ambayo alishindwa kujieleza fedha hizo ni za nini na anatarajiwa
kufikishwa mahakamani September 9," amesema Makungu.
Ametoa
rai kwa watumishi wa umma kuridhika na vipato wanavyopata kwa waajiri
wao na wananchi watoe taarifa ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu au namba
ya dharura 113 ambayo wananchi hapaswi kulipa.
"Wananchi
fanyeni hivyo ili kuwaondoa watumishi wachache ambao bado hawaridhiki
na kipato halali wanacholipwa na mwajiri," amesema Makungu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara Holle Joseph Makungu akizungumza mjini Babati na waandishi wa habari.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...