Na,Jusline Marco;Arusha


Chama cha wanahabari wanawake Tanzania(TAMWA)kimewaomba viongozi wa taasisi za dini kutoa elimu katika jamii kuhusu umuhimu wa wanawake katika kuondoa vikwazo vinavyowakabili wanawake katika zoezi la uchaguzi mkuu 2020.


Aidha takwimu zinaonesha kuwa asilimia 37 ya wanawake ndio walioko katika ngazi za maamuzi bungeni lakini bado yapo mapengo katika ushiriki wao ikiwemo lugha dhalilishi wakati wa uchaguzi zinazowakatisha tamaa wanawake kuwania nafasi za uongozi.


Akizungumza katika Mkutano wa Viongozi wa Dini na Siasa,Kuhamasisha Amani na Haki Tanzania,Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Bi.Rose Reuben amesema changamoto nyingine ambayo inawakumba wanawake ni uteuzi usiozingatia jinsia ndani ya vyama vya siasa,hofu na kuyojiamini kwa baadhi ya wanawake wenye nia ya kugombea na ilani za vyama zisizozingatia jinsia.


"Mapengo mengine ama changamoto zilizobainika ni pamoja na rushwa ya ngono inayotajwa kutumika wakati wa uchaguzi,rushwa ya fedha,uchumi duni kwa wanawale wanaotaka kugombea na hivyo kupelekea kushindwa kufanywa kampeni,mila na desturi kandamizi zinazowazuia wanawake wasishiriki katika siasa."Alisisitiza mkurugenzi wa TAMWA


Ameongeza kuwa ushiriki wa wanawake katika siasa na katika ngazi za maamuzi ni eneo lililo na changamoto lukuki hivyo linahitaji kuhimizwa na viongozi wa ngazi za juu,asasi za kiraia,wanawake wenyewe na viongozi wa dini.


"Ipo mitazamo hasi katika jamii kuwa mwanamke anapoingia katika siasa basi amejishushia heshima na hadhi yake kwani hakuumbwa kuwa kiongozi,hayo yote yanachangia kupunguza idadi ya wanawake viongozi".Aliongeza mkurugenzi huyo


Vilevile ameongeza kuwa TAMWA inaendelea kuhimiza umuhimu wa wanawake kushiriki siasa na katika ngazi za maamuzi kwani ndiyo wanaoaminika katika jamii ambapo viongozi wa dini wameombwa kutumia nafasi zao katika kuhimiza jamii kuondoa mila na mitazamo potofu inayochochea ushiriki duni wa wanawake katika siasa na katika ngazi za maamuzi.


Pamoja na hayo ameelwza kuwa kutokana na Tanzania kusaini mikataba mbalimbali inayolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa na mikataba mbalimbali ya amani,hivyo taasisi za dini kutoa elimu kuhusu ushiriki wa wsnawake katika siasa ili kuondoa vikwazo na mitazamo yote potofu inayozuia ushiriki wa wanawake katika siasa na kutoa mafundisho yanayomuonyesha mwanamke kama shupavu na mleta mabadiliko ili kuwajengea wanawake kujiamini.


Awali akifungua Mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta amesema kuwa serikali itashughulika na watu wanaotoa lugha dhalilishi kwa wanawake ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini kuhamasisha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.


“Jambo hilo la akina mama limekuwa ni kilio kikubwa sana ambapo hata uchaguzi ukipita lazima Arusha waonyeshe mfano katika kuhamasisha wanawake na kukemea vikwazo vyote vinavyozuia wanawake kushiriki katika uongozi kupitia viongozi wa dini wa wilaya zote 6 sita za mkoa wa Arusha na serikali kwa ujumla” Alisema Iddy Kimanta.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati za amani Tanzania  shekhe Alhad Musa Salum ambaye pia ni shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake huonekana kutumiwa na vyama vya siasa katika uhamasishaji wa kuongeza wanachama na sio kugombea.


“wanawake wanakabiliwa na changamoto ikiwemo kuonekana hawawezi chochote lakini tunaona vitabu vyetu vya dini jinsi wanawake walivyoshiriki mambo mbalimbali na kuyafanikisha mfano katika Biblia tunamuona Debora, Esta Mariamu na wengine wengi” Alisema  Shekhe Alhad.


Ameongeza kuwa kwa mujibu ya sensa iliyofanyika mwaka 2012 zaidi ya asilimia 51 ni wanawake ambapo asilimia 30 tu ndio wanaoshiriki katika uongozi na shughuli zingine kutokana na sababu mbalimbali zinazowazuia ikiwemo mfumo dume, mila kandamizi, lugha dhalilishi na mambo mengine.


“wanawake wanaweza hivyo tujaribu kuondoa hivi vizuizi na mfano mzuri tunamuona makamu wa Raid mama Samoa Suluhu alivyotoshe katika nafasi yake wengine ni mawaziri wanawake spika wa bunge aliyepita Anna Makinda, Asha Rose Migiro na wengine wengi”


Naye mwenyekiti wa kamati za amani Mkoa wa Arusha Askofu Dkt.Solomon Masangwa Askofu wa kanisa la KKKT dayosisi  ya Kaskazini kati  amesema kuwa  mwanamke ni mtu muhimu sana katika kila jamii na kila taifa kwani wananafasi kubwa katika ulinzi na ustawi wa taifa akipewa kuongoza na kunukuu neno kutoka kitabu cha Yeremia 31; 22.


Askofu Masangwa amefafanua kuwa Mungu amemfanya mwanamke kuwa sehemu kubwa ya wakala wa uumbaji katika ulimwengu huu pamoja na kuwa mtunzaji wa familia na wanapopewa nafasi ni lazima washughulike masuala ya ustawi.

Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,katika ni Mwenyekiti wa kamati za Amani Mkoa wa Arusha Dlt.Solomon Masangwa pamoja na  mwenyekiti wa kamati za Amani Taifa Shehk Alhad Musa Salum wakiwa katika mkutano wa viongozi wa Dini na Siasa Kuhamasisha Amani na Hali Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...