Na Farida Saidy, Michuzi Tv Morogoro
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imewataka Watanzania kuchangamkia fursa zitokanazo na ufugaji wa wanyamapori kwa kuanzisha Bustani za wanyamapori (zoo), Mashamba ya ufugaji wa wanyamapori (wildlife farm), pamoja na Ranchi za ufugaji wa wanyamapori (wildlife ranch) ili kujiongezea kipato chao na taifa kwa ujumla.

Akitoa elimu kwa wananchi kupitia chombo kimoja cha habari hapa nchini juu ya ufugaji wa wanyamapori Muhifadhi wa wanyamapori kutoka TAWA, Bi. Vero Mollel amesema moja ya  taratibu za kuanzisha miradi ya ufagaji wa wanyamapori ni Kuwa na Hati ya umiliki wa eneo linalokusudiwa kwa ajili ya ufugaji  lisilopungua  hekta 2000 kwa Ranchi.

Hata hivyo amesema faida za ufugaji wa wanyamapori ni pamoja na kuongeza kipato cha Taifa kwa kuongezeka kwa fedha za kigeni hapa Nchini kupitia utalii, kukuza mbegu za wanyama, pamoja na kupunguza utegemezi wa wanyamapori kwenye maeneo yaliohifadhiwa. 

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa chanzo kikuu kinachotegemewa  na Mabucha ya Nyama Wanyamapori hapa nchini ni Ranchi na mashamba ya Wanyamapori, uvunaji wa wanyamapori kwenye maeneo ambayo wamezidi na kuleta madhara kwa binaadamu (cropping) pamoja na uwindaji wa kitalii.

Katika hatua nyingine amewataka wale wote wanaotaka kuanzisha Mabucha ya nyama za wanyamapri kufika katika ofisi za mamlaka hiyo  ili kuweza kupata utaratibu wa namana ya kuendesha mabucha hayo bila ya kukiuka sheria na miongozo iliyowekwa na mamlaka.

Ikumbukwe kuwa  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ilianzishwa mwaka 2014 chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Kuhifadhi wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009 ikiwa ni shirika la umma chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...