Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS,) David Ndibalema akikabidhi leseni na vyeti kwa mmoja wa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa ubora baada ya kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.


Baadhi ya wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa ubora wakifuatilia mjadala maalumu baada ya kukidhi matakwa ya viwango kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.


SHIRIKA La Viwango Tanzania (TBS) limetoa leseni na vyeti 167 kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa ubora baada ya kukidhi matakwa ya viwango kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS,) David Ndibalema amesema vyeti na leseni hizo ni za bidhaa za vyakula,vipodozi, vifaa vya ujenzi,vilainishi,vitakasa mikono,vifaa vya umeme, vifaa vya makenika, magodoro pamoja na Vifungashio.

Aidha Ndibalema ameishukuru Serikali kwa kuwahudumia wajasiriamali wadogo kupitia huduma za TBS juu ya udhibiti ubora bila malipo ya gharama za ukaguzi na upimaji.

"Wajasiriamali hawa wataendelea kuhudumiwa bure kwa kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo. Hata baada ya miaka mitatu kuisha,TBS itafanya tathimini ya uwezo wa wajasiriamali ili kupima uwezo wao wa kulipa". Amesema Ndibalema.

Hata hivyo Ndibalema amewataka wazalishaji hao kuendelea kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango kwa mustakabali wa afya na mazingira ya watumiaji kwa ujumla.

Amesema, kwa  mahitaji ya kusajili jengo la biashara  tovuti ya TBS tayari ina  mfumo wa kujisajili kwa njia ya mtandao kwa kuweka taarifa  na kuweza kupata akaunti  itasaidia kupata huduma ambazo hutolewa na TBS katika mfumo wa mtandao.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa kampuni ya Woiso Original Products, wanaoshughulika na utengenezaji wa viatu Joachim Komba amesema, kampuni yao inajivunia kupata cheti kutoka TBS kwani itatanua wigo kwa wateja wao kuwaamini na kutumia  bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.

Vilevile, Afisa Masoko wa kiwanda cha Yehehe Investment Limited, Godlisen Mwanjala amesema mteja anapohudumiwa na wafanyabiashara anatakiwa aridhie kwa kuoneshwa leseni ili kujihakikishia bidhaa hiyo anayonunua imekidhi viwango na inafaa kwa matumizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...