Na Agness Francis, Michuzi TV
KATIKA kuendeleza soka la Tanzania na kufikia hadhi ya kimataifa, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania( TFF) limesaini mkataba na kampuni ya six international Ltd ili kujenga vituo bora vya mpira hapa nchini.
Zoezi hilo la kusaini makubaliano hayo ya ujenzi wa vituo hivyo limefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za TFF.
Makubaliano hayo yamelenga mradi huo utakaotekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya Kigamboni, Kigamboni technical center, pamoja na Mkoani Tanga, Tanga technical center.
Mradi huo utajengwa kwa kutumia fedha za FIFA na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12, mara baada ya kuanza kwa ujenzi huo.
Aidha Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa miradi hiyo inakwenda kwa awamu na matarajio yake ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na vituo hivyo vya mpira.
"Mradi unakwenda kwa awamu, na katika mipango yetu tutahakikisha kila Mkoa unakuwa na kitu kama hicho,Tutatumia fedha za wadau wetu mbalimbali pamoja na wale watakaojitokeza pia." Amesema Wallace Karia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...