Kufuatia kukosa soko la uhakika kwa zao la mahindi kwa wakulima wa Ludewa mkoani Njombe na kupelekea kuuza mahindi hayo kwa bei ya sh. 350 mpaka 250 kwa kilo hatimae tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi.

Ufumbuzi huo umepatikana baada ya mbunge mteule wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kufikisha kilio hicho cha wakulima kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hasan alipowasili jimboni humo kwa ziara ya kampeni ya kumuombea kura Rais John Magufuli.

Makamu huyo wa rais amesema kuwa baada ya kupewa taarifa hiyo aliwasiliana na Wakala  wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) bila kuchelewa na kupewa majubu kuwa kabla ya ijumaa ijayo watakuwa  wameweka ofisi kwa ajili ya kununua mahindi hayo kwa bei ya sh. 530 mpaka 550 kwa kilo.

"Baada ya kupewa taarifa juu ya tatizo hili la soko la mahindi muda huo huo nikafanya mawasiliano na NFRA ambapo nao wamelipokea kwa haraka na kuanza utekelezaji", Alisema makamu wa Rais.

Sambamba na hilo pia mh. Samia amesema wapo katika mkakati wa kujenga maghara yenye uwezo wa kuhifadi tani nyingi zaidi za mazao mbalimbali ambayo yatajengwa katika vijiji vya Shauri moyo na Mundindi wilayani humo.

Aliongeza kuwa maboresho mengine ni katika sekta ya mifugo ambapo zaidi ya shilingi milion miatisa na nane kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa.

Aidha kwa upande wa wananchi wamemshukuru mbunge huyo kwa kuwafikishia kilio chao hicho kwani angalau kwa sasa wanaweza  kuona faida ya kilimo hicho.

Julius Haule ni mmoja wa wakulima wa wilaya hiyo amesema kuwa wamekuwa wakitumia gharama nyingi katika kilimo lakini faida hakuna.

" Tumekuwa tukitumia gharama kubwa Sana katika kununua mbolea, mbegu, na kuweka wasaidizi mashambani lakini ukivuna unakutana na bei ndogo ya mahindi kitu ambacho inakubidi kuuza hivyo hivyo kwakuwa ninashida na pesa lakini ukipiga hesabu unajikuta umetumia gharama nyingi kulima kuliko faida uliyopata baada ya kuvuna", Alisema Haule.

 Mbunge mteule jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Chama na mkoa.

 Makamo wa Rais Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi katika kijiji cha Ilela kilichopo wilayani Ludewa mkoani Njombe baada ya kuwasili akitokea mkoa wa Ruvuma

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Njombe na wilayani Ludewa wakiserebuka wakati wakimsubiri kumpokea makamo wa Rais mama Samia Suluhu Hasan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...