Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Kigoma
WAGOMBEA ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Kigoma wamewaomba wananchi wa mkoa huo kuhakikisha katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, kura zote ziende kwa Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli.

Wamesema kwamba mambo maubwa ambayo yamefanyika katika Mkoa wa Kigoma katika kipindi cha miaka mitano, heshima pekee ambayo wanatakiwa kuionesha basi iwe ni Dk.Magufuli kushinda kwa kishindo.

Wakizungumza leo Septemba 17, 2020, wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Magufuli wagombea hao wamefafanua Mkoa wa Kigoma katika kipindi cha miaka mitano yamefanyika maendeleo makubwa yakiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Mengine yaliyofanyika ni elimu bure kwa shule msingi hadi sekondari ,ujenzi wa vituo vya afya, hositali , uunganishaji umeme katika vijiji mbalimbali vya Mkoa huo pamoja na kuimarisha nyanja nyingine za kiuchumi,kijamii na kimaendeleo.

Akimuombea kura Dk.Magufuli, Mgombea ubunge Jimbo la Buhingwe Dk.Philip Mpango amesema katika miaka mitano Serikali imeimarisha uchumi na ndio maana kuna mambo makubwa ya maendeleo yamekuwa yakifanyika.

Pia amesema Dk.Magufuli aliamua kuteua wabunge watatu wa mkoa wa Kigoma kuwa katika baraza lake la mawaziri ili kumsaidia kazi , hivyo ameomba wananchi wa Mkoa huo kura zote ziende kwa Mgombea urais wa CCM."Tunataka Dk.Magufuli ashinde kwa asilimia 100 katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako amesema Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano amefanya mambo ya kutukuka, hivyo katika uchaguz mkuu wa mwaka huu ni vema wakamchagua tena ili aendeelee kufanya kazi ya kuleta maendeleo ambayo ameifanya kwa mafanikio makubwa.

Profesa Ndalichako ameongeza katika elimu chini ya uongozi wa Rais Magufuli Serikali imeendelea kutoa elimu bure na hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi na sekondari

Wakati wa Kigoma, amesema Serikali imejenga shule ya msingi na sekondari,vyuo vya Ufundi kwa baadhi ya wilaya,ujenzi wa hosteli nchi nzima zaidi ya 600, maktaba za kisasa kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi na ujenzi wa nyumba za walimu.

Amesisitiza Dk.Magufuli amefanya mengi,ameonyesha unyenyekevu mkubwa katika kuhakikisha nchi inakuwa na maendeleo huku akifafanua Wilaya ya Kasulu barabara ya kilomet 260 imejengwa kutoka Kibingo hadi Manyovu.

"Wananchi wa Mkoa wa Kigoma niwaombe kura zote za Urais ziende kwa Dk.Magufuli ili akaendelee kutekeleza ahadi zake pamoja na kuendelea kukamilisha yale ambayo ameanza kuyafanya."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...