KATA ya Vikindu wamezindua rasmi kampeni leo, nawanachi wameshauriwa kuchagua chama cha mapinduzi ili wapate maendeleo.
Akizungumza mbele ya wandishi wahabari wakati akifungua kampeni ya CCM kata ya vikindu akiyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya mkuranga Juma Abeid amesema hakuna anaweza kushindana na Magufuli katika maendeleo.
"Ukiangalia ilani ya chama cha mapinduzi inatosha kuleta maendeleo kwa miaka mitano ya uongozi wake vijiji 23 vya vikindu vinawaka umeme, Mpaka Sasa vikindu tunashule ya msingi shirikishi na kituo cha afya kinajengwa ili kupunguza changamoto za afya." amesema Abeid
Aidha mpaka Sasa Ulega amesha jenga zahanati zaidi ya 40 na nane zitafunguliwa kipindi cha kampeni
Hata hivyo amemuasa mgombea huyo wa udiwani kuhakikisha kuwa nawatumikia wananchi wote na sio kuwa bwana mkubwa kwa jamii.
Aidha amemtaka kuondoa makundi na dharahu baina yao ili kuhakikisha analeta maendeleo Kwa wanavikindu na Mkuranga kwa ujumla.
"Usiwe diwani wa watu, acha ubaguzi kawe kiunganishi kwa Watu wa vikindu na halmashauri ya kuranga." Amesema Abeid
Kwa upande wake Ally Msikamo amewata wanaCCM kutojibweteka na badala yake wapambane kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda Kwa kishindo.
Aidha amewataka wanachama wa jimbo la Mkuranga kuondoa makundi na kusimama kwapamoja kukipigania chama.
Nae Mke wa ugombea ubunge jimbo la Mkuranga Mariam Ulega amewaomba wanachi wote wa Mkuranga ifikapo Oktoba 28,2020 kura zote kwa Ulega, Magufuli na madiwani wa chama cha mapinduzi.
Mohamed Maundu ni mgombea udiwani kata ya vikindu amewahidi wananchi wa Vikindu kuwa akishinda atafanya kazi kwa bidii na atapigana kwa hali na mali kuhakikisha halmashairi ya Mkuranga kusonga mbele.
Aidha ameongeza kuwa atasimamia changamoto zote za Vikindu kuhakikisha kata hiyo inasonga mbele katika huduma zote za kijamii ikiwemo miundo mbinu na kusimamia mikopo kwa vijana na kinamama ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Abeid akimdai Mgombea Udiwani kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, Mohamed Maundu alipozindua Kampeni za CCM leo Septemba 4, 2020.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza wakati alipozindua Kampeni za CCM Kata ya Vikindu leo Septemba 4, 2020.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo akisisitiza jambo.
Mke wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza na wananchi wa kata ya Vikindu wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM leo Septemba 4, 2020.
Mgombea Udiwani kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, Mohamed Maundu akiwaomba kura wananchi wa kata hiyo wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM leo Septemba 4, 2020.
Sehemu ya Viongizo mbalimbali wa CCM.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...