Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano  kwa Umma wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Lilian Mpanju Rugaitika akizungumza na mwananchi wakati alipotembelea banda la TIA maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Mpanju amesema maobesho hayo yamesaidia kusogeza huduma kwa wanafunzi na kupata taarifa mbalimbali na baadhi ya wanafunzi wamepata udahili moja kwa moja katika banda hilo.


Mwakilishi wa Wanafunzi waTaasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Said Majujuka akiwapa uzoefu wa wanafunzi kujiunga na Taasisi hiyo kutokana mikakati ya ufundishaji uliopo katika taasisi hiyo  wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda la TIA katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Mkutubi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Magreth Mwamaso akizungumza na mwanafunzi aliyetembelea Banda la TIA maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Mkutubi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) France Mwambene akitoa maelezo kwa wanafunzi wakati walipotembelea Banda la TIA katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wakifanyiwa udahili katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania katika maonesho ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Wakuu wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
 Makamu  Mkuu wa  Chuo- Mipango , Fedha na  Utawala wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Matei Mapunda akitoa maelezo kwa wafanyakazi wanaotoa huduma katika maonesho ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu  wa  Chuo- Taaluma, Ushauri na  Utafitivwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) Dkt.Momole Kasambala  (mwenye suti) akizungumza kuhusiana na maonesho ya Vyuo vikuu yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, katikati ni Makamu wa Chuo- Fedha na Utawala Dkt.Matei Mapunda kulia ni  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Lilian Mpanju.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...