Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja Barafu uliopo Mto wa Mbu wilayani Monduli kuzindua Kampeni za CCM wilayani humo, Septemba 2, 2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Zelote Stephene . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa vazi la CCM na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa wakati alipozindua kampeni za CCM wilayani Monduli katika uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, Septemba 2, 2020. Kulia ni Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Monduli Fred Lowassa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipozindua kampeni za CCM wilayani Monduli kwenye uwanja wa Barafu Mto wa Mbu , Septemba 2, 2020.
WANAMONDULI
HAKIKISHENI CCM INASHINDA-MAJALIWA
MJUMBE wa Kamati Kuu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amevunja makundi
ya wanachama wa CCM walioomba uteuzi wa kuwania ubunge katika jimbo Monduli
mkoani Arusha na kuwataka washirikiane katika kuhakikisha chama kinapata
ushindi wa kishindo.
Pia, Mheshimiwa
Majaliwa ametumia fursa hiyo amewaomba wakazi wa wilaya ya Monduli mkoani
Arusha na Watanzania wote bila kijali itikadi zao wamchague Rais Dkt John Pombe
Magufuli ili aendeleze kazi ya kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.
Waziri Mkuu ameyasema hayo
leo (Jumatano, Septemba 2, 2020) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya
Monduli, Arusha kwenye mkutano wa kampeni za CCM kumuombea kura Rais Dkt.
Magufuli pamoja na wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani wa CCM.
“Kazi iliyonileta hapa ni
kuwaomba kura wana Arusha na wanaMonduli naomba kura zenu zote bila ya kujali
itikazi za vyama vyenu tumpigie kura Mheshimiwa Rais Magufuli na mgombea ubunge
Fredrick Lowassa na wagombea wote wa udiwani kupitia CCM.”`
Amesema wananchi
wanajua kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Rais Dkt. Magufuli, hivyo amewaomba wamchague tena kwa kuwa miradi mikubwa
ya kimkakati aliyoitekeleza kwenye maeneo mbalimbali nchini imegusa wananchi
wengi.
Kadhalika,
Mheshimiwa Majaliwa amesema Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 imeweka
msisitizo kwa Serikali kuleta
mageuzi ya utalii, kilimo, mifugo na uvuvi
ili kuwa na uhakika wa chakula na kujitegemea
kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu
katika maendeleo ya uchumi.
“Tutahakikisha uzalishaji unaongezeka katika sekta ya mifugo, utalii na uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija katika kilimo,
ufugaji na uvuvi ili kuchochea maendeleo ya uchumi, hasa katika sekta za viwanda na huduma za jamii. Fugeni kisasa mpate faida na Serikali ya CCM itaendelea
kuwaunga mkono.”
Amesema tayari vijana wengi wamenufaika kupitia sekta hizo, hivyo
ni lazima Serikali iendelee kuziboresha zaidi. Pia Serikali imepanga kuongeza
idadi ya watalii wanaoingia pamoja na kuongeza pato litokanalo na sekta hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...