Na Pius Ntiga, Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idi KIMANTA amesema katika kipindi Cha miaka mitano zaidi ya shilingi Trilioni Moja zimepelekwa Mkoani humo kwa ajili ya huduma ya  maendeleo  ikiwa ni kiasi kikubwa Cha fedha zilizopelekwa tofauti na mikoa mingine nchini.


Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha ametoa kauli hiyo  leo wakati akizungumza na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM Mjini Arusha.


Katika Mahojiano hayo Kimanta amesema kiasi hicho Cha fedha kilichopelekwa Mkoani humo kuanzia mwaka 2015-2020 ni kikubwa mno tofauti na mikoa mingine hivyo akampongeza Rais John Magufuli kwa upendo wake kwa wananchi wa Arusha.


Amesema kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 500 zimetumika katika mradi Mkubwa wa kimkakati wa Maji utakaohudumia wananchi wa Mji wa Arusha na vitongoji vyake, ambao umeanza kunufaisha wananchi wa Arusha ambao wameupongeza.


Aidha Kimanta amesema  kila mwaka fedha za maendeleo zimekuwa zikiongezeka ambapo shilingi Bilioni 58 ni kwa ajili ya miradi ya  barabara na shilingi 

Bilioni 70 kwa ajili ya Afya zimekuwa zikiufikia Mkoa huo.


Pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha amesema jumla ya shilingi Milioni 900 zimepelekwa kwa ajili ya miradi mikubwa ukiwemo ule wa Maji Mkubwa Arusha na barabara ikiwemo ya Baypas.


Pamoja na Mambo mengine amesema Elimu bure hadi Sasa mkoa umepokea kiasi Cha shilingi  bilioni 170 kwa ajili ya elimu bure kwa shule za Msingi na hali hiyo imeongeza hali ya ufaulu na idadi ya wanafunzi shuleni.


Amesema  idadi ya wanafunzi imeongezeka na kuleta changamoto ya idadi ya madarasa Mkoani Arusha, ambayo wanaendelea nayo kuitafutia ufumbuzi.


Aidha,  jumla ya  Bilioni 6 amesema zimeletwa Arusha kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe ikiwemo Iriboru.


Pia amesema Hospitali za wilaya zinajengwa na hivyo kufanya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kutekelezwa vizuri ikiwemo sekta ya utalii.

 

Kuhusu sekta ya utalii amesisitiza kwa Sasa ipo vizuri licha ya janga ya maambukizi ya virus vya Corona kuukumbamkoa wa Arusha na maeneo mengine nchini.


"Sekta ya Utalii  ipo vizuri na inaiingizia Pato zuri Taifa na Mkoa wa Arusha kwa ujumla" alisema Mkuu wa Mkoa.


Kuhusu Hali ya ulimzi na usalama Mkoani Arusha amesema  Ni nzuri na amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kusimania vizuri hali ya ulinzi.


Akizungumzia kuhusu Uchaguzi mkuu Kimanta amesema hadi sasa shughuli za kampeni zinaendelea vizuri kwa vyama vya siasa kuendelea kunadi Sera zao katika mikutano ya  kampeni ambayo inahudhuriwa kwa wingi na wananchi.


Aidha amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kupiga kura OKTOBA 28 mwaka huu kwani hali ya ulinzi umeimarishwa vizuri.


"Wananchi wanajitokeza kwa wingi kuhudhuria mikutano ya kampeni na wana matumaini kuwa Oktoba 28 wananchi watajitokeza kwa wingi bila bughudha kwenda kupiga kura". alisema Kimanta.


Kuhusu Ujio we Reli amesema  imeunufaisha mkoa wa Arusha kupitia Treni ambayo ilisimama zaidi ya miaka 30 umri ambao Ni wa mtu nzima.


"Mwezi iliyopita Mkoa wa Arusha ukipata Treni ya kwanza ya Mizigo baadye Treni ya Abiria ambayo itachochea huduma za ukuaji wa uchumi wa wananchi na Mkoa kwa ujumla"


Amesema Treni ya kwanza ilileta mzigo ambao ungebebwa na malori zaidi ya 80 lakini ukaletwa na Treni na hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe kubwa kwa wanachini wa Arusha.


Kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli vimechochea ukuaji wa uchumi na Pato la wananchi wa Arusha.


 vilivyotolewa na serikali mkuu huyonwa Mkoa wamesema Biashara nyingi ya.mkoa huu IPO kwenye minadana Sasa kero wafanyabiashara wagodo hawazipati Tena Jijini Arusha.


Amesema wafanyabiashara hao Sasa wanafanya shughuli zao vizuri bila vitisho vyovyote na kwamba shilingi Blioni 22 za  makusanyo ya mkoa tangu 2015 hadi sasa ni ongezeko la asilimia 53 yaani mara mbili umeongezeka ukiwemo mchango wa wafanyabiashara wadogo.


"Matarajio ya wanaarusha 2020-2025 ni makubwa kwa  wanachinwa Arusha na  watarajie Arusha itapaa zaidi tofauti na ilivyo Sasa na watatoa Asante Oktoba 28 mwaka huu.


Pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha amewata Wananchi watunze kadi zao za kumpigia Kura na wakapige bila wasiwani wowote kwani hali ya ulinzi umeimarishwa mwanzo na baada ya Uchaguzi mkuu Jijini Arusha.


Amewataka pia Viongozi wa vyama vya siasa wafanye kampeni kwa staha na watumie lugha ambazo hazitaleta  chuki  kwa wananchi.


Wakati huo huo, Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi, Mrisho Gambo, amewataka wananchi kuzipuuza wa Arusha kupuuza ahadi zinazotolewa na wanasiasa wa upinzani akiwemo Godbless Lema ambaye yupo kwenye harakati za kuaga kwani Hana chake tena Oktoba 28 mwaka huu.

 

Amesema utendaji kazi wake uliotukuka akiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha unampa jeuri ya kushinda katika Uchaguzi mkuu ujao kwani aliwatumikia kwa moyo wake wote wanaarusha.


"Nawaomba Kura zenu wananchi wa Arusha Mjini Octoba 28 mnichague kwa Kura nyingi ili tuendeleze maendeleo ya Arusha"  alisema Gambo.

 Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi, Mrisho Gambo akieleza mambo mbalimbali na namba alivyojipanga alipokuwa akifanya mahojiano na  mmoja wa Watangazaji wa kipindi cha Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM Mjini Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idi KIMANTA alipokuwa akizungumza na mmoja wa Watangazaji wa kipindi cha Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM Mjini Arusha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...