Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

CHAMA Cha Waajiri Tanzania (ATE) wanatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 60 toka kuanzishwa kwa chombe hicho kinachofanya kazi ya kuwakilisha na kutetea maslai ya waajiri nchini katika masuala ya kazi na Ajira.

Maadhimisho hayo yatakuwa mwanzoni wa Mwezi Disemba na Katika maadhimisho haya kutakuwa na shughuli mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema amesema mbali na maadhimisho hayo pia wamezindua
kampeni yenye lengo la kuongeza uelewa miongoni mwa Waajiri nchini kuhusiana na umuhimu wa Uanagenzi pamoja na programu nyingine za mafunzo mahala pa kazi.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa wahitimu ili kutengeneza fursa Ajira na kupelekea vijana wengi kuwa na sifa za kuajirika.

Ameeleza, ATE kwa kushirikiana na Serikali, Shirika la Kazi Duniani (ILO) na wadau wengine kama Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini(TPSF) wameendelea kutoa mchango mbalimbali ili kuendeleza ujuzi nchini ikiwemo kuwahamasisha waajiri kuwa na programu za mafunzo ya kuendeleza ujuzi mahali pa kazi kama uanagenzi na Mafunzo kwa wahitimu.

Aidha Dkt Mlimuka amesema, lengo ni kuwapatia mafunzo kwa vijana ya kuwajengea uwezo wa kuajiriwa, Kuandaa miongozo ya uendeshaji wa programu ya uanagenzi pamoja na mafunzo mengine ya ujuzi mahala pa kazi.

"Tumejenga mahusiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zinazojishulisha na kuendeleza ujuzi kwenye maeneo ya kazi mfano Mwaka 2016 tuliingia rasmi kwenye ushirikiano na Mtandao wa kimataifa wa Uanagenzi (Global Apprenticeship Network )," amesema.

"Waajiri watapata faida kwa kushiriki katika Programu hii ya uanagenzi ikiwa ni kutengeneza wafanyakazi wenye ujuzi katika kampuni kwa kuwapa mafunzo ya ujuzi wa kazi katika nadharia na vitendo, kufanikisha mahitaji ya kampuni na kuhakikisha kampuni ina wafanyakazi wenye ujuzi wa kutosha katika sekta husika," amesema Dkt Mlimuka.

ATE ni mmoja kati ya wadau wa UTATU wa Shirika la Kazi Duniani Pamoja na Serikali na Shirikisho la vyama vya wafanyakazi ambapo wamekuwa wakishugulikia kutatua masuala yote yanayohusiana na mahusianao kazini na sheria za kazi kwa sekta husika katika ngazi ya kitaifa nchini

GAN ilianzishwa rasmi mwaka 13 ili kutatua tatizo kubwa la Ajira kwa vijana duniani pia kama njia ya kuwajengea ujuzi vijana kwa mustakabali wa kazi za baadae. GAN ni muunganiko wa makampuni, taasisi mbalimbali Pamoja na vyama vya Waajiri duniani ambazo zimejizatiti kutekeleza mafunzo ya kuendeleza ujuzi katika maeneneo ya kazi lengo likiwa ni kutengeneza fursa za Ajira kwa vijana na ujuzi stahiki.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni yenye lengo la kuongeza uelewa miongoni mwa waajiri nchini kuhusiana na umuhimu wa uanagenzi pamoja na  Programu nyingine za mafunzo mahala pa kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...