Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM,) Abdallah Ulega ambae pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wa jimbo  la Mkuranga ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake katika jimbo hilo.


Na Grace Gurisha, Michuzi TV

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkuranga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), Abdallah Ulega, amesema kujengwa kwa barabara za Wilaya za Mkuranga na Kisarawe, kwa kiasi kikubwa zitasaidia kukuza uchumi wa wananchi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.

Aidha, amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anaziunganisha Wilaya hizo kwa barabara yenye hadhi ya Mkoa ili kuondoa ulazima wa wananchi wa maeneo hayo kuzungukia jijini Dar es Salaam.

Ulega amesema hayo Oktoba 11, 2020 wakati akiendelea na kampeni zake katika jimbo hilo huku akiwaomba wananchi wampigie kura zote za ndiyo ili aweze kutimiza azma yake hiyo ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

"Barabara  hii ina umuhimu mkubwa na kwamba endapo itajengwa, kwa asilimia kubwa itawaondolea usumbufu waendaji wa wilayani wakiwemo wasafiri kutoka mikoa ya Morogoro na kwingine ambao kwa sasa huwalazimu kuingia Dar es Salaam kwanza ndipo wafike huko." amesema Ulega.

Ulega ambaye ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema mtu anayetoka Rufiji, Kibiti au hata Mikoa ya kusini na kutaka kwenda Kibaha au Morogoro,kama hana kazi ya kumpeleka Dar es Slaam hata hitaji kufika huko, atapita Mkamba, Mzenga, Msanga hadi Mlandizi na kwenda  Morogoro, kwa hiyo barabara hii itakuwa chachu ya maendeleo.

"Lengo langu na Serikali ya CCM naamini kwamba kwa kukamilika kwake kutawawezesha wananchi wa wilaya hii waliopo vijiji vyote vitakavyopitiwa na barabara hiyo ambao watasafirisha mazao yao kwa urahisi na kuwaondolea adha wanayoipata." amesema.

Pia, Ulega amewataka wananchi wa vijiji hivyo kuongeza juhudi ya kilimo kwa kulima mazao mengi ya chakula na biashara  ili kujiinua kiuchumi kwa kuwa uhakika wa usafirishaji wa mazao hayo kwenda Mikoa mingine utakuwepo kutokana na ujio wa barabara hiyo.

Aidha, katika hatua nyingine Ulega amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ameweza kuviunganisha na nishati ya umeme sehemu kubwa ya Wilaya hiyo  vikiwemo vijiji vya Chamgoi, Mbulani  na  Mkelezange, ambapo kwa sasa wanaendelea kuviunganisha vijiji vya Kibuyuni, Mkuluwili, Ndoleni, Kibunguchana, Kikundi hadi Kibesa.

Amesema hatua hiyo inatokana na uchapakazi wa Rais Dkt.John Magufuli, huku akiwaahidi wananchi wa Mkelezangu kuwa kijiji hicho kitakuwa kimeunganishwa na kuwashwa umeme huo kabla ya Oktoba 28, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...