Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw Theobald Sabi akizungumza na wadau wa sekta binafsi  kuhusu mchango na huduma za benki hiyo katika kuinua sekta binafsi nchini wakati wa Mkutano maalumu ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa jitihada zake katika kuiboresha sekta  hiyo katika kipindi cha miaka mitano. Wanaoshuhudia  ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Bi Angela Kairuki (Kulia) na  Katibu Mkuu wizara ya viwanda na biashara, Prof. Riziki Shemdoe (Katikati).

Viongozi waandamizi wa Benki ya NBC akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw Theobald Sabi (wa tatu kulia) pamoja na Meneja Mahusiano Serikalini wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) William Kallaghe (wa pili kulia) wakifuatilia mkutano maalumu ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa jitihada zake katika kuiboresha sekta  hiyo katika kipindi cha miaka mitano.

 

Meneja Mahusiano Huduma Binafsi wa benki hiyo Bw  Mark Peter (kulia) akilezea kuhusu huduma za benki hiyo kwa  mmoja wa wadau wa sekta binafsi  Bw Elias Lukumay  kutoka  Chama Cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) waliotembelea banda la benki hiyo wakati wa mkutano maalumu ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa jitihada zake katika kuiboresha sekta  hiyo katika kipindi cha miaka mitano.

Maofisa wa benki ya NBC akiwemo  Meneja Mahusiano Huduma Binafsi wa benki hiyo Bw  Mark Peter (wa tatu kulia) wakilezea kuhusu huduma za benki hiyo kwa baadhi ya wadau wa sekta binafsi waliotembelea banda la NBC wakati wa mkutano maalumu ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa jitihada zake katika kuiboresha sekta  hiyo katika kipindi cha miaka mitano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...