Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) hii leo imezindua mwezi wa Huduma kwa Wateja wake huku ikisisitiza kuendelea kuzingatia weledi katika utoaji wa huduma zake sambamba na kuboresha zaidi ushirikiano wateja wake.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya mwezi mmoja iliyoanza leo, ilishuhudiwa wafanyakazi pamoja na watendaji wakuu wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi wakiwakaribisha kwa kuwapigia makofi ya heshima wateja wa benki hiyo waliokwenda kupata huduma kwenye tawi la Makao Makuu jijini Dar es Salaam.Wateja pia walionesha kufurahishwa na heshima hiyo.

“Tumetenga mwezi mzima kwa ajili ya huduma maalum kwa wateja wetu kwa kutambua na kuthamini nafasi yao muhimu katika kuifanya Benki ya NBC kuwa benki kubwa na yenye faida zaidi nchini. Hii inakuja wakati ambapo pia tumewekeza zaidi katika kuwapatia huduma nzuri na rafiki kwao,’’ alisema Bw Sabi alipokuwa akifungua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam.

Aidha benki hiyo imejipanga kuutumia mwezi huo wa Huduma kwa Wateja kama fursa nzuri ya kuboresha zaidi muonekano wake kwa mamia na maelfu ya wateja wake kote nchini.

"Mafanikio tunayojivunia leo ni kwasababu ya wateja wetu waliotuamini wameendelea kuwa waaminifu kwa muda mrefu, ndiyo sababu tunasherehekea nao pamoja. Kwa miongo kadhaa, tumeunda uhusiano mzuri na wateja wetu wanaokua haraka kimafanikio na tunaendelea kujitolea kuwapatia suluhisho za kifedha za ubunifu na zenye uwajibikaji, ambazo zinawawezesha kuendelea kukua zaidi '' Aliongeza.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Bi Salama Musa alisema katika kipindi chote cha mwezi huo shughuli kadhaa zimepangwa kwa ajili ya wateja wa ndani na nje katika kuthamini na kuimarisha zaidi mahusiano ya pande zote mbili.

"Katika kipindi chote cha mwezi huu, tutatembelea vituo kadhaa vya afya, tutatoa zawadi kwa wateja wetu mbalimbali, tutatembelea wateja wetu ili kupata maoni yao juu ya huduma zetu pamoja na kuendelea kutoa mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali,’’ alisema.

Wakizungumzia huduma za benki hiyo baadhi ya wateja walisema wameguswa na benki hiyo sio tu katika kuhifadhi pesa zao au maswala ya mkopo bali pia benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.

"Kimsingi ni kwamba ninafurahia sana huduma za Benki ya NBC. Imekuwa ni kwa kipindi cha muda mrefu nimekuwa nikishirikiana na benki hii na kiukweli ninaridhishwa zaidi na utamaduni wao wa kazi na maadili ya taaluma yanayotoa fursa kwangu kuendelea kufanya kazi pamoja katika kufanikisha shughuli zangu. Nimejenga nyumba zangu kupitia mikopo ya benki hii na kwa hilo nawashukuru sana.’’ alisema Bw Maulid Kitenge, Mteja wa benki hiyo ambae pia ni mwandishi mashuhuri wa habari za michezo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kushoto) akishirikiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo kukata keki wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo iliyofanyika tawi la makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na  Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Bi Salama Musa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya wateja binafsi, benki ya NBC Makao Makuu Bw Elibariki Masuke (Kushoto)

 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Katikati) akiwaongoza wafanyakazi na viongozi waandamizi wa benki hiyo kuwakaribisha wateja  waliofika kupata huduma za kibenki tawi la  benki hiyo makao makuu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo. Wanaoshuhudia ni pamoja na  Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Bi Salama Musa (wa pili kushoto)


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw Maulid Kitenge wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...