


CHANGAMOTO za wizi wa fedha ,utapeli na dhuluma zilizokuwa zikiwakabili wakulima wa mazao ya kimkakati huenda sasa zitafika kikomo baada ya Benki ya CRDB kupata ufumbuzi wa changamoto hizo kwa kuanzisha akaunti maalumu ya Fahari Kilimi maalumu kwa wakulima.
Wakati dunia ikiwa katika wiki ya huduma kwa wateja iliyobeba kauli mbiu ya “Dream Team” Mashirika ya umma ,ya binafsi pamoja na taasisi mbalimbali za fedha nchini zimeungana katika maadhimisho ya wiki hii huku CRDB wakiweka wazi namna ambavyo wamejipanga kumsaidia mkulima.
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Kaskazini Chiku Issa amesema wakulima katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakipokea fedha zao kwa njia ya pesa taslimu .
“Hili limetokea zaidi maeneo ambayo yana mazao ya kimkakati kama Pamba ,Kahawa,Tumbaku,Chai na Katani ,wengi wa wakulima hawa walikuwa wanapokea kwa njia ya Cash”alisema Chiku .
“Kulikuwa na ubadhilifu mkubwa watu walikuwa hawapewi fedha zao sahihi laikini pia ilikua ni hatari sana wengi wao walikuwa wanapoteza fedha kwa matapeli lakini pia kwa kuibiwa” aliongeza Chiku.
Amesema CRDB imekuja na bidhaa nyingi tofauti ambazo zinagusa jamii kwa kila kada ambapo akaunti ya kilimo ni maalumu kwa wakulima na kwamba haina makato ya aina yeyote na itasaidia kuendeleza kilimo.
Chiku amesema CRDB itaendelea kuboresha huduma zake ili kila mtanzania na kila mteja wa CRDB ziweze kumgusa na kuweza kupata mikopo kwa urahisi ili kuboresha maisha yao na kwenda na uchumi wa kati.
“Benki inaungana na taasisi nyingine duniani kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwahudumia na kuwahamasiha kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hii ili kuboresha maisha yao.”alisema Chiku.
Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa kila mwaka ifikapo mwezi Oktoba ambapo taasisi,mashirika na kampuni mbalimbali huadhimisha kwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida iliyopatikana.
Mwisho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...