Meneja wa Mkoa wa Kihuduma Kisarawe DAWASA Erasto Mbwambo akisaidia kushusha mzigo walipotembelea kituo cha Kisarawe Orphanage Centre na kutoa msaada wa chakula.

Mmiliki na Mlezi wa Kituo cha Kisarawe Orphanage Centre Veronica Kilango (kulia) akipokea msaada wa Chakula kutoka kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Kisarawe Erasto Mbwambo (wa pili kushoto) na Afisa Mahusiano Dawasa Joseph Mkonyi (wa pili kulia) wakushuhudiwa na Afisa Ustawi wa Jamij Kisarawe Teofrida Mbilinyi (kushoto) baada ya kutembelea kituo hicho leo Kisarawe, Mkoani Pwani.

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha Kisarawe Orphanage Centre, Mmiliki na Mlezi Veronica Kilango na Afisa Ustawi wa Jamii Kisarawe Teofrida Mbilinyi
Afisa Mahusiano Dawasa Elizabeth Eusebius akipata maelezo  ya bidhaa zinazotengenezwa na watoto wa Kituo cha Kisarawe Orphanage kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii Kisarawe Teofrida Mbilinyi, Dawasa wametembelea kituo hicho kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani.

 Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) wakipata maelezo ya kina ya Kituo cha Kisarawe Orphanage Centre, kutoka kwa  Afisa Ustawi wa Jamii Kisarawe Teofrida Mbilinyi (wa pili kushoto). Dawasa wametembelea kituo hicho na kutoa msaada wa Chakula

 
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

MBALI na kutoa huduma ya Maji kwa wananchi, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wametoa msaada wa chakula kwa kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Kisarawe.

Kituo hicho cha Kisarawe Orphanage Centre kina watoto takribani 29 kutoka maeneo mbalimbali.

Akizungunza kwa niaba ya Kituo hicho, Afisa Ustawi wa Jamiii Kisarawe Teofrida Mbilinyi amesema kituo hicho kinalea watoto wa aina tofauti na sio Yatima peke yake.

Teofrida amesema, wana watoto waliokuwa wanaishi kwenye mazingira magumu, watoto walio na kesi ambao hawawezi kulala mahabusu hata wale waliofanyiwa a na ukatili wa kijinsia.

"Kituo hiki kinalea watoto wa aina mbalimbali, sio yatima peke yake bali hata sisi tunakiamini na tunamletea watoto waliokuwa na kesi ambao hawawezi kulala mahabusu, waliofanyiwa ukatili wa kijinsia na hata wale tuliowaokota," amesema.

"Mmiliki wa kituo hiki anatambulika, tunashirikiana nae na hata yeye ndiye anayemleta mtoto (mtuhumiwa) kwenye kesi yake na pia anatambulika kisheria," ameeleza Teofrida.

Mmiliki wa Kituo hicho, Veronica Kilango ameeleza kituo hicho kilianza mwaka 2012 na alirithi kazi hiyo kutoka kwa baba yake na alianzia kwenye nyumba ya kupanga hadi sasa amepata eneo la kudumu.

Veronica amesema, wana watoto jumla 29, wanaoanzia elimu ya awali hadi kidato cha Sita ila wapo ambao walipita hapo na wapo Vyuoni huku wengine wakisomea fani za ufundi.

"Tunawashukuru sana Dawasa, nilipoambiwa wanakuja nilidhani wanakuja kutukatia maji lakini ujio wenu ni mzuri, mmeonesha moyo leo naamini watoto watafurahi kwa hiki mlichotuletea," amesema Veronica.

Afisa Mahusiano Dawasa, Joseph Mkonyi amesema wametoa mchango huo kidogo kwa kituo hicho ili kiwasaidie watoto hao na huu ni mwanzo kwani Kwa sasa Dawasa wanatoa huduma Kisarawe.

Pia, amesema wanafanya shughuli mbalimbali za mikono ikiwemo kutengeneza asali, mafuta ya mnyonyo, viatu vya ngozi na kutengeneza mabatiki.
 
Katika kutembelea na kutoa msaada kwenye kituo hicho, msafara uliongozwa na Meneja wa Dawasa Kisarawe   Erasto Mbwambo, Afisa Rasiliami watu Kisarawe Benatus  Kazoba Afisa Mahusiano Dawasa Joseph Mkonyi, David Mkulila na Elizabeth Eusebius.

Dawasa wametoa msaada wa Mchele, unga wa sembe, maharage, mafuta ya kula, Sukari na sabuni ya kufulia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...