WAZIRI Mkuu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM,) Kassim
Majaliwa amesema Serikali ijayo ya CCM itaendelea kuwaunga mkono na
kuwaendeleza wajasiriamali wakiwemo wasanii.
"Serikali
ya CCM inawathamini sana wasanii kwa sababu sanaa ni sawa na ujasiriamali. Kwa
maana hiyo, sanaa ni ajira," amesema.
Majaliwa ametoa
kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Oktoba 2, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa
wilaya ya Kahama katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Magufuli mjini
Kahama, mkoani Shinyanga.
Akielezea
kuhusu ujenzi wa barabara za kuunganisha mikoa, Majaliwa amesema
kwenye ilani ya uchaguzi, barabara kubwa inayotajwa kuunganisha mji wa Kahama
na mikoa ya jirani ni ya kutoka Katavi hadi Tabora kupitia Ugalla.
"Katika
uk. 73, Ilani yetu inataja barabara zinatotakiwa kuanza kujengwa kwa kiwango
cha lami ambazo ni Mpanda - Ugala - Kaliua - Ulyankulu - Kahama (km 428); Geita
– Bukoli – Kahama (km 107) na Kahama – Nyamilangano – Uyogo (km 54).”
Majaliwa ambaye amemaliza ziara yake ya kumuombea kura mgombea Urais kwa tiketi
ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli amemnadi pia mgombea ubunge wa jimbo la Kahama
mjini, Bw. Jumanne Kishimba na wagombea udiwani wa wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Madini, Bw. Dotto Biteko amesema wilaya ya
Kahama imepanda chati ya makusanyo yatokanayo na madini kutokana na usimamizi
wa Serikali ya awamu ya tano.
"Kwenye
makusanyo ya madini, Kahama ilikuwa ikishika nafasi ya nne. Sasa hivi imepanda
na kuchukua nafasi ya pili. Mnashindana na Geita. Chunya ndiyo ilikuwa ikishika
nafasi ya pili, lakini sasa hivi mmeiacha mbali. Chagueni viongozi wa CCM ili
iendelee kuwaletea neema," amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...