Na Agness Francis, Michuzi tv.

KUELEKEA mchezo wa derby ya Italia itakayopigwa kesho majira ya saa moja usiku , Ac milan dhidi ya Intermilan, Mshamuliaji wa  Ac milani Zlatan Ibrahimovic atakuwa katika kikosi hicho kuumana na watani wao wa jadi katika mchezo huo wa serie A.

Mshambuliaji huyo amerejea tena uwanjani ambapo sasa yupo tayari kwa mapambano ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi na mashabiki wa timu hizo zote mbili.

Zlatan amekuwa akisugua  benchi toka mwezi septemba  baada ya kugundulika ana maambukizi ya virusi vya corona COVIDE 19.

Huku shambuliaji wa zamani wa Intermilan Vieri akiwa ana matumaini  makubwa na Zlatan licha ya kutocheza kwa muda mrefu, anaamini anakiwango cha  hali ya juu ambacho atakidhihirisha kwenye mchezo huo.

"Uzoefu wake sio wa kutiashaka  anakila kitu, Ufundi wake namna anavyoutazama mchezo, kufunga na kutoa pasi za magoli na kufanya timu yake kucheza vizuri ni vitu vikubwa."Amesema Vieri alipofanya mahojiano na  Lagazzetta dell sport.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...