KAMPUNI ya simu, Infinix Mobility LTD inayotamba na toleo jipya aina ya Infinix HOT 10 imeendelea kuongeza mashabiki kupitia kampeni inayohusisha ushindani kuimba kupitia  #HOT10RapChallenge kupitia simu hiyo inayosifika kwa kukaa na charge kwa muda mrefu (5200mAh.)

Infinix kupitia simu zao wamekuwa wakishirikiana na wasanii mbalimbali katika kampeni zao na kupata tuzo kutoka “Guinness World Record” ya video ndefu iliyoshirikisha wasanii mbali mbali kutoka nchi zaidi ya 50 duniani, akiwemo rappers Brian Simba na Eddy Super kutoka Tanzania, video hio ilifanyika kwa njia ya mitandao na rappers walionyesha ujuzi wao.

Kampuni hiyo ikaendelea kuleta mashindano ya mtandaoni maarufu kama “Online Challenge” iliyopata washiriki zaidi ya 100 katika mtandao wa Instagram wakiwania zawadi ya Infinix HOT 10 na fedha taslimu Tsh 300,000.

Joshua Joram ambaye ni mwanafunzi wa chuo ni mmoja wa wateja wa Infinix HOT 10, alisema, “Infinix wanajua kutupatia sana maana wanaleta simu zenye uwezo mkubwa kwa gharama nafuu ambazo hata mwanafunzi wa chuo anaweza kujibana mwenyewe tu na kununua sio kama brand nyingine,

Infinix HOT 10 imekuwa ni mkombozi kwa sisi wanafunzi uwezo wake wa kudumu na chaji kwa muda mrefu pasipo na haja ya kuzima data inatusaidia sisi wanafunzi kujisomea mtandaoni lakini pia inatupa nafasi ya kuchangamsha akili na games mbalimbali kutokana na processor ya MediaTek Helio G70 kuweza kuhimili games zenye ujazo wa aina yoyote”.

Pamoja ya kuwa ni simu pendwa kwa vijana wa kisasa lakini bado kampuni hiyo haijaacha tamaduni yake yakufanya kampaini kwa njia ya promosheni ili kujiweka karibu zaidi na wateja wake na kwa sasa ukitembelea duka lolote lenye promotion ya Infinix HOT 10 TUPO live basi pindi tu ununuapo bidhaa ya Infinix HOT 10 unapewa zawadi ya blender, kinga’amuzi au headphone papo hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...