Mwanasheria na Mratibu wa Mradi wa kuwezesha Jamii kuhusiana na Sheria na Haki za Ajira Mkoa wa Dar es Salaam wa Kituo Cha Msaada wa Kisheria cha Wanawake na Watoto (WILAC) Consolata Chikoti akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kituoa hicho kinavyotoa huduma katika kusaidia upatikanaji wa Haki kwa wananchi.


*WILAC kusaidia wafanyakazi hao msaada wa kisheria ya kupata Haki

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

KAMPUNI  kubwa ya usafishaji Taka na Usafi wa  Mazingira ya jijini Dar es Salaam imekiuka mkataba wa ajira kwa wafanyakazi wake na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kukosa haki zao.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Usafishaji Taka na Usafi wa Mazingira wamefika katika Kituo Cha Msaada wa Kisheria cha Wanawake na Watoto (WILAC) kwa ajili ya kutaka Msaada wa Kisheria   kutokana na kukaa muda mrefu bila mwajiri kampuni hiyo kuwa majibu kuhusiana na kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi Habari Mwanasheria na Mratibu wa Mradi wa kuwezesha Jamii kuhusiana na na Sheria na Haki za Ajira Mkoa wa Dar es Salaam Consolata Chikoti amesema kuwa baadhi ya wafanyakazi hawana uelewa katika suala la sheria wakati wanaingia mikataba ya kufanya kazi.

Amesema wafanyakazi wa Kampuni hiyo walifika na kutaka msaada na hatua mbalimbali zinaendelea huku akisema hawezi kutoa jina la kampuni hiyo mpaka pale tararibu zitakaporuhusu.

Chikoti amesema kuwa wamekuwa wakipata wateja wengi katika kampuni na viwanda huku wengine wakiwa wamepata haki kabla ya kufika katika hatua za kimahakama.

Chikoti amesema kupitia Mradi huo uliofadhiliwa na  Legal Services Facility (LSF) wameweza kuzunguka sehemu mbalimbali kutoa elimu katika masuala ya sheria na Haki za ajira kwenye viwanda na kampuni.

Hata hivyo amesema kuwa baadhi ya waajiri nao wamekuwa wanashindwa kutekeleza masharti ya mikataba.

Amesema WILAC itaendelea kutoa uelewa katika masuala ya sheria na Haki za ajira Ila jamii iweze kuwa na uelewa katika kujenga utu sehemu za kazi kwa kuzingatia mikataba iliyowekwa kisheria.

Chikoti amesema kuwa inapotokea watu wanataka msaada wa Kisheria  na kutaka meza ya mazunguko mwajiri akikataa tararibu zingine zinafuata katika vyombo vinavyohusika na ikishindikana wanakwenda mahakamani.

"Nia ya msaada wa kisheria ni kujenga ustawi kwa waajiri na wafanyakazi kila mmoja kujua wajibu kwa matakwa ya Kisheria yaliyowekwa na nchi."amesema Chikoti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...