Kikundi cha wazee wa kata ya Lugarawa wilayani Ludewa mkoani Njombe wamemuasa mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kutokaa kimya bungeni bali aeleze  matatizo ya jimboni kwake.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli kiongozi wa wazee hao Emmanuel Mtweve alimkabidhi mbunge huyo zawadi ya mbuzi aina ya beberu pamoja na jogoo zilizoambatana na ujumbe huo.

"Mtoto wetu Kamonga, tunakupa huyu jogoo ili akuamshe asubuhi na mapema! Ukisikia sauti yake usilale , na huyu beberu ukiwa bungeni upaze sauti yako wananchi wako tusikie unavyo tutetea maana sisi tunakuamini na tutafurahi zaidi ukitusemea shida zetu bungeni", Alisema Mtweve.

Aliongeza kuwa wabunge wengi wa Ludewa  wamekuwa wakiongoza kipindi kimoja tu na kuondolewa hivyo kwa sasa wanayo furaha kwa kumpata mbunge kijana na mwenye sifa zote ambazo wao wanazihitaji.

"Mbunge tuliyempata sasa ni mbunge wa kuongoza vipindi zaidi ya vitano hivyo tunahakika kijana huyu ataleta mabadiliko makubwa sana katika wilaya yetu, sisi wazee tumemkubali na tunampa baraka zote", Alisema Mtweve.

Aidha kwa upande wa mbunge mteule Joseph Kamonga aliwashukuru wazee hao na kusema kuwa imani hiyo waliyonayo kwake ni deni kubwa sana ambalo anatakiwa kulilipa ipasavyo.

Aliahidi kuwatumikia wananchi hao kwa kadri ya uwezo wake huku akiwaomba wananchi hao kumtuma popote katika kusaka maendeleo.

Wakati huohuo mbunge huyo alipokuwa njiani kuelekea katika mkutano mwingine kijiji cha Mkiu kata ya Lubonde akiwa njiani alisimamishwa na wanakikundi cha Uhunzi kilichopo katika eneo hilo la Mkiu.

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzie Mwenyekiti wa kikundi hicho Andrea Chakula alisema kuwa wamemsimamisha mbunge huyo kwa lengo la kumfahamisha shughuli zao na kumzawadia moja ya zana wanazotengeneza.

Alisema kikundi hicho kina wanachama 17 na kinajihusisha na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya magari pamoja na pikipiki.

Mhunzi huyo alimpa mbunge pamoja na diwani mteule wa kata hiyo Edga mtitu kifaa mfano wa shoka huku akiwaeleza kuwa amewapa kifaa hicho ili kiwe ulinzi kwao wa kupambana na vikwazo vitakavyojitokeza.

"Tunawakabidhi vifaa hivi mfano wa shoka ili muweze kupambana na changamoto mbalimbali ikiwe magugu hivyo kifaa hiki kitawasaidia kufyeka magugu hayo na kupata njia ya kupita", Alisema Chaula.

Kwa upande mwingine mbunge huyo alipokuwa kwenye mkutano katika kijiji cha Mkiu kata ya Lubonde aliwataka wananchi kumchagua Rais Magufuli kwakuwa ana mipango mingi ya kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara ambapo mpaka sasa anatekeleza ujenzi wa barabara ya kiwango cha zege inayoanzia Lusitu mpaka Mawengi kwa km. 50 ambapo zimetumika bilioni 167.
Sambamba na barabara hiyo pia kuna barabara nyingine za kiwango cha lami kutoka Itoni mpaka Manda, Mkiu mpaka Madaba na barabara itakayounganisha miradi mikubwa ya Liganga na Mchuchuma.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkiu huku wengine wakiwa na shauku ya kushikwa mkono na mbunge huyo  baada ya kuwasili kijiji hapo kwa aajili ya kufanya mkutano wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli.
Kiongozi wa kikundi cha wahunzi Andrea Chaula (kushoto) akimkabidhi mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga  zawadi ya kifaa mfano wa shoka.
Diwani mteule wa kata ya Lubonde Edga mtitu akipokea zawadi ya kifaa mfano wa shoka kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha wahunzi Andrea Chaula.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwapungia mikono wananchi(hawapo pichani) wa Kijiji cha Mkiu kata ya Lubonde alipofanya mkutano katika kijiji hicho. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (kushoto) akiwa na diwani mteule wa kata ya Lubonde Edga mtitu wakimpokea mwanachama wa CHADEMA Stelius Thomas aliyeamua kujiunga na CCM katika kata ya Lubonde.
Diwani mteule wa kata ya Lubonde Edga mtitu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkiu katika kata ya Lubonde.

Mzee Emmanuel Mtweve (kushoto) akimuasa mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamongap(Mwenye t-shirt nyeupe) huku akimkabidhi zawadi ya kuku aina ya jogoo na mbuzi aina ya beberu.


 

Wananchi wa Kijiji cha Mkiu kata ya Lubonde wakimshangilia mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga pamoja na diwani mteule wa kata ya Lubonde Edga Mtitu(hawapo pichani) walipofanya mkutano katika kijiji hicho wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli.
Kikundi Cha ngoma ikitumbuiza mbele ya mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipowasili kufanya mkutano katika kata ya Lugarawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...