Na, Lusajo Frank DSJ
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Etienne Ndayiragije ametangaza leo mchana kikosi kitakacho ivaa timu ya taifa ya Burundi (Intamba m'Urugamba), October 11 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.
Ndayiragije ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachoingia kambini Octoba 5, kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki.
Kwa upande wa makipa ni Metacha Mnata anayeidakia timu ya (Yanga SC), Aishi Manula (Simba SC), pamoja na David Kisu wa (Azam FC)
Ambapo mabeki ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussein kutoka katika kikosi cha wekundu wa msimbazi (Simba SC), Israel Mwenda (KMC FC), Brayson David, Abdallah Sebo (Azam FC), Bakari Mwamnyeto (Yanga SC) Dickson Job (Mtibwa Sugar) na Iddy Mobbi kutoka katika timu (Polisi Tanzania).
Viungo wakiwa ni Jonas Mkude, Said Hamisi, Yassin Mzamiru (Simba SC), Himid Mao (ENPPI SC, Egypt), Iddy Nado, Salum Abubakar (Azam FC), Feisal Salum (Yanga SC), Ally Msengi (Stellenbosch FC, South Africa).
Huku Washambuliaji ni John Bocco anayeichezea (Simba SC), Mbwana Samatta (Fenerbahce FC, Turkey), Nickson Kibabage, Simon Msuva (Diffa El by Jadidi, Morocco), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo) akiwemo na Ditram Nchimbi anaelisakata kabumbu kunako kikosi cha viijana wa jangwani(Yanga SC).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...