Katibu Mstaafu  wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  January Makamba amewaomba  watanzania Ifikapo Oktoba 28,2020, wahakikishe wanamchagua kwa kura nyingi  Rais Magufuli kutokana na rekodi yake ya utekelezaji wa ilani na sera za CCM kwa miaka mitano iliyopita


Ombi hilo amelitoa wakati wa kampeni za  kumnadi na kumuombea kura Mgombea  Ubunge Jimbo la Korogwe vijijini Timotheo Mzava zilizofanyika viwanja vya soko la  Mombo.


Makamba alisema  Chama Cha Mapinduzi ni bora zaidi kuliko vyama vingine vya upinzani  sababu CCM  haiwezi kupeleka Mgombea wa ngazi yeyote  mwenye shaka shaka  kuhusu sifa zake na uwezo wake .


Makamba ambaye pia ni Mbunge aliyepita bila kupingwa alisema  kila mmoja anajua utendaji kazi wa Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, hivyo wamchague tena ili  aweze kudhihilisha matunda yake na  kumalizia kazi zilizobakia .


Alisema kuwa Matunda ya kazi alizozifanya Rais Magufuli na ambaye ni mgombea wa CCM yanakwenda kudhihirika zaidi  atakapopewa  nafasi nyingine ya kushindilia , kuimarisha na kumalizia  pale alipopaanza.


"CCM ikimteua mtu  kuwa mgombea wake wa ngazi yoyote ujue mtu huyo kachujwa vya kutosha kwani Chama chetu hakiwezi  kupeleka kwa wananchi  mgombea ambaye ana shaka shaka kuhusu sifa na uwezo wake"Alisema Katibu huyo Mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa

 Mbunge Mteule wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba  alipokuwa akizungumza na Wananchi 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...