
Na Amiri Kilagalila, Njombe
JUMLA ya Makundi 16 ya waangalizi wa nje wapewa fursa na vibali vya kufuatilia mwenendo wa shughuli ya uchaguzi Tanzania huku asasi za kiraia na taasisi 97 za ndani pia zikipata nafasi hiyo.
Amebainisha hilo Kamisha wa tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Mary Longway wakati wa mkutanao na wadau wa uchaguzi uliofanyika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeruhusu watazamaji wa ndani na nje,katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambapo imetoa vibali kwa asasi za kiraia na taasisi 97 za ndani na vibali kwa makundi 16 ya watazamaji wa nje” alisema Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi
Anasema “Siku ya uchaguzi vyama vya siasa vimepewa nafasi ya kuweka wakala katika kila kituo cha kupigia kura,wakala atakuwepo kituoni kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa uchaguzi zinazoendelea kituoni pale na kama zinazingatia sheria,kanuni,taratibu na maelekezo yanayotolewa na tume,lengo kubwa ni kulinda maslahi ya Chama na wagombea wake”amesema Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi
Hata hivyo amesema “Tayari vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi,vimepata nakala tepe ya orodha ya wapiga kura waliomo katika orodha ya daftari la kudumu la wapiga kura hii ni kuwawezesha mawakala kutimiza wajibu wa kuhakiki wapiga kura wanaofika kituoni” Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi
Jaji mstaafu Mary Longway amesisitiza kuwa “Tume inasisitiza umuhimu wa vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeni zao,ikwemo kuepuka Lugha za kashfa,maneno ya uchochezi yanayotishia usalama na amani ya Nchi” Jaji mstaafu Mary Longway
Aidha amesema“Wakati tume inaendelea kuratibu,kusimamia na kuendesha uchaguzi huu kwa kutumia sheria za uchaguzi.Vyama vya siasa,wagombea na wananchi wanakumbushwa kuwa katika kipindi hiki sheria nyingine za nchi hazijasimama” Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi
Amewahakikishia wananchi kuwa tume itaendelea kufuata katiba na sheria katika utekelezaji wa majukumu yake.
“Tume inawahakikishia wananchi kuwa,imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata katiba,sheria,kanuni na miongozo mbali mbali na inaamini kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu basi watanzania wataweza kupiga kura kwa amani” Jaji mstaafu Mary Longway Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...