Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema benki ya Nmb iendelee kutoa elimu wa huduma hizo mpya ili ziweze kuwasidia wakulima na wananchi kwa ujumla
Akizindua wiki ya huduma kwa wateja ambayo inafanyika kila mwaka amesema wateja wanahitaji kupata huduma bora hivyo iendelee kuboresha zaidi huduma hizo
Naye Meneja wa Nmb tawi la Tandahimba Julietha Ndazi amesema wameanzisha huduma mpya tatu ambazo ni whatsapp namba ambayo itamsidia mteja kupata ufafanuzi wa huduma za Nmb
Amesema ingine ni QR Code ambayo inatoa nafasi kwa wateja kutoa mapendekezo ya uboreshaji wa huduma za kibenki na huduma ya tatu ni huduma ya kurudisha token ya Luku kwa wateja ambao wamenunua umeme kupitia NMB mkononi
" Huduma ya kurudisha token ya luku ilikuwa na changamoto kwa wateja wetu lakini kwa sasa tatizo hilo tumelitatua kabisa kea kuanzisha huduma hiyo"amesema Ndazi
Aidha naye Afisa Mikopo Godluck Mteri amesema mbali na huduma hizo zipo huduma za Bima mbalimbali ambazo zinatolewa na benki hiyo hivyo wakulima na wananchi wachangamkie fursa hiyo ili kuzilinda mali zao kwa kuzikatia bima

Dc Sebastian Waryuba akizindua wiki ya huduma kwa wateja Nmb tawi la Tandahimba

Meneja wa tawi la Nmb Tandahimba Julietha Ndazi akifafanua huduma mpya walizoanzisha kwa wateja wao

Afisa Mikopo wa benki hiyo Godluck Mteri akielezea faida ya huduma ya Bima inayotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Makampuni husika

Washiriki na watumishi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...