Msimu wa 11 wa mbio za Rock City Marathon zinazofanyika kila mwaka jijini Mwanza umezinduliwa rasmi hii leo jijini Dar es Salaam.

Waandaaji wa mbio hizo Kampuni ya Capital Plus International imesema kuwa mbio hizo zenye agenda ya kutangaza utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa zimepangwa kufanyika Novemba 29 mwaka huu eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi huo, Mratibu wa mbio hizo Bw Kasara Naftal alisema maandalizi muhimu yameshafanyika ikiwemo suala zima la fulana za washiriki pamoja na medali huku akitaja mbio zitakazohusishwa kuwa ni km 21, km 10 na Km 5.

“Kuhusu zawadi, pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 2 kila mmoja, sh.mil 1.3 /- kwa washindi wa pili na sh. 700,000 kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na zawadi za medali na pesa taslimu.’’

“Kwa upande wa mbio za Kilomita 10 hatutakuwa na zawadi za fedha taslimu isipokuwa washiriki watajipatia medali na tshirts . Kuhusu mbio za kilomita tano ambazo zitahusisha washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporates) sambamba na washiriki wenye ualbino zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi watatu wenye ualbino pekee.’’ Alitaja

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka kumi na moja iliyopita zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Kampuni ya Ujenzi ya CRJE, Pigeon Hotel, CF Hospital, Hospitali ya Bugando, Garda World, The Cask na Chuo cha SAUT Mwanza.

Kwa upande wake Msemaji wa mbio hizo Bw Samwel Gisayi alisema usajili wa mbio hizo tayari umekwisha anza kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya mbio hizo pamoja na usajili wa kawaida kupitia vituo mbalimbali vilivyopo mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Dodoma, Arusha huku mikoa zaidi ikiendelea kuongezwa.

“Usajili unaendelea vizuri na mwitikio wa washiriki ni mkubwa. Lengo ni kukimbiza washiriki wasiopungua 3000 yakiwemo makundi yote yaani wakimbiaji wa mbio za ushindani (Elite runners), washiriki wa mbio za kujifurahisha (Fun run) pamoja na wanafunzi.” Alisema.

Waratibu wa mbio za Rock City Marathon Bw Naftal Kasala (wa pili kulia) na Bw Samwel Gisayi (Kushoto) sambamba na wawakilishi kutoka vilabu vya wakimbiaji wa mbio za marathon Bi Caroline Joseph (wa pili kushoto) na Bw Mustafa Abdulhafidhi (Kulia) wakionesha fulana kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo msimu wa 11 zinazotarajiwa kufanyika Novemba 29 mwaka huu jijini Mwanza, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo.

Mratibu wa mbio za Rock City Marathon Bw Naftal Kasala (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu msimu mpya wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Novemba 29 mwaka huu jijini Mwanza, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo. Kushoto ni Msemaji wa mbio hizo Bw Samwel Gisayi.

Msemaji wa mbio za Rock City Marathon Bw Samwel Gisayi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu msimu mpya wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Novemba 29 mwaka huu jijini Mwanza, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam hii leo.


Wadau wa mbio za Rock City Marathon wakiwemo wawakilishi wa vilabu vya wakimbiaji pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi huo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...