Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Imeelezwa kuwa zaidi ya bilioni 8 zimetumika kwa ajili ya miradi ya umeme wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ambapo Kati ya fedha hizo bilioni 5 kwa ajili ya mradi wa gridi ya taifa na bilioni 3 kwa ajili ya mradi wa rea.

Hayo aliyasema mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga katika mkutano wa kumuombea kura rais John Pombe Magufuli na kuongeza kuwa lengo la serikali ya Rais John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya umeme.

" Umeme ni kitu muhimu Sana kwa maendeleo ya taifa letu endapo tutampa miaka mitano mingine Rais Magufuli ataweza kukamilisha miradi hiyo na kuhakikisha wananchi wote wanakuwa katika maendeleo zaidi", Alisema Kamonga.

Katika hatua nyingine mbunge huyo amesema ataendeleza majengo ya chuo Cha veta kilichopo Shaurimoyo Katika kata ya Lugarawa wilayani humo ambacho kimesahaulika kwa kipindi kirefu ambapo kwa kufanya hivyo kitakuwa msaada mkubwa kwa vijana.

Aliongeza vijana wengi wamekuwa wanashindwa kupata ujuzi mbalimbali wa kiufundi na kadhalika kitu ambacho kinapelekea vijana hao kujiingiza katika makundi yasiyo faa.

Alisema endapo chuo hicho kitakamilika kitaleta maendeleo makubwa kwa vijana ambapo watakuwa na uwezo wa kujiajili na kuajiliwa pia.

Sanjari na hayo pia alizungumzia moja ya barabara za kiwango cha rami  zilizopangwa kutekelezwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi  2020 - 2025 ni kutoka mkiu, Lugarawa, Mundindi, mavanga mpaka madaba .

Alisema barabara hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kwakuwa itawawezesha kusafirisha mazao yao kwa uraisi zaidi.

Aidha kwa upande wa mgombea  ubunge viti maalum mkoa wa Njombe balozi Pindi chana alisema wananchi wanapaswa kuhamasishana kwenda kumpigia kura Rais Magufuli ili aweze kupata kura za kutosha.

Aliongeza kuwa vyama vingine havina muelekeo unaoeleweka hivyo endapo watapiga kura kwa vyama hivyo watakuwa wamepoteza kura yao.

Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa na mbunge viti maalum mkoa wa Njombe Balozi Dk. Pindi Chana katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Lugarawa kata ya Lugarawa
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Mbugani kata ya Mavanga
Wakazi wa kata ya kata ya Lugarawa wakiwa wameshika trei la mayai pamoja na kuku aina ya jogoo na tetea kwaajili ya kumkabidhi mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alipofanya mkutano katika kata hiyo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba akiwa na mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, Mbunge viti maalum mkoa wa Njombe Balozi Dk. Pindi Chana, Diwani wa kata ya Mavanga Daud Daniel pamoja na wajumbe wa kamati ya kampeni wilaya wakiserebuka katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mbugani
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akisalimiana mzee katika kijiji cha Amani kata ya Mundindi wilayani Ludewa


Wakazi wa Kijiji cha Mavanga kilichopo kata ya Mavanga wakimsikiliza mbunge mteule jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (hayupo pichani)
Mbunge viti maalum mkoa wa Njombe Balozi Dk. Pindi Chana akiwa na mbunge mteule wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga wakisindikizwa na wananchi wa kijiji cha Amani kilichopo katika kata ya Mundindi wilayani Ludewa
Mbunge mteule wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akitoa shukrani kwa wakazi wa kata ya Lugarawa baada ya kumpa zawasi ya trei la mayai na kuku aina ya jogoo na tetea
Mbunge viti maalum mkoa wa Njombe Balozi Dk. Pindi Chana akiwa na mbunge mteule jimbo la Ludewa Joseph Kamonga pamoja na Diwani wa kata ya Mundindi Wise Mgina wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kata ya Mundindi wakionyesha ishara ya miaka mitano mingine kwa Rais John Pombe Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...