Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga aliyepita bila kupingwa amemtaka mgombea mwenza wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu kuwaomba radhi wana Ludewa kwa kusema uongo hadharani.

Mbunge huyo ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadahara katika kata ya Lupanga wilayani Ludewa na kuongeza kuwa mgombea huyo amesema kuwa wananchi wanadanganywa kuwa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kinafanya siasa juu ya ujenzi wa barabara ya kiwango Cha zege inayoendelea kujengwa kwa kutoka Lusitu Hadi Mawengi alipofanya mkutano wake siku ya Jana katika kata ya Mlangali.

Alisema  Rais Dk. John Magufuli amewekeza katika barabara hiyo bilioni 167.5 ili wana Ludewa waweze kupata maendeleo.

"Wananchi wa Ludewa wanajitambua hivyo hawawezi kudanganyika kwa vitu ambavyo wanaviona kwa macho! hivyo Chadema wajipange upya juu ya sera zao kwa Ludewa kwa hili wamefeli", Alisema Mbunge Kamonga.

Aliongeza kuwa wananchi wanawaona wakandarasi walivyo na kasi ya kuijenga barabara.

Alisema Rais Dk. Magufuli amefanya Maendeleo makubwa sana katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu bure ambapo ametoa zaidi ya bil. 29 afya zaidi ya bilioni 3 n.k

"Hivi kwa fedha zote hizi ambazo Rais Magufuli amewaletea kwa ajili ya maendeleo unafikiri utawaambia nini wakakuelewa?", Alisema Kamonga.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM pamoja na wananchi wakimpokea mbunge wao aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga Katika kata ya Lupanga
Wajumbe wa kamati ya kampeni wilaya wakiserebuka walipowasili kata ya Lupanga Kijiji Cha Lupanga. Wakwanza kushoto ni Stella ngairo, Ednda Haule  na Leah Mbilinyi ambaye pia ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ludewa
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa Kijiji cha Mapufya
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba akiwa na mbunge wa Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba ( katikati) akiselebuka na baadhi ya viongozi wenzie na wanachama wa Chama hicho katika kata ya Lupanga
Mkazi wa kata ya Lupanga akionyesha furaha yake kukutana na mbunge aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga (wakwanza kulia) akiongea na wananchi wa kijiji cha Lupanga Mapufya. Anayefuata diwani wa kata hiyo Dominicus Mganwa, diwani wa kata ya Mawengi Leodgar Mpambalioto wote wamepita bila kupingwa na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ludewa
 Mbunge wa jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akiongea na wananchi wa kijiji cha Lupanga kilichopo kata ya Lupanga Wilayani Ludewa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...