Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu ameahidi kusukuma upatikanaji wa Umeme wa Rea na Kuboresha Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari katika kata ya Marungu.

Ummy akiinadi Ilani ya Ccm na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Kata ya Marungu iliyo pembezoni mwa Jiji la Tanga, amesema Ilani ya Ccm imeeleza kufikisha umeme katika maeneo ya pembezoni kupitia kwakutumia REA (Mpango wa Umeme Vijijini)hivyo endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha maeneo ya Amani,Mkembe na Marungu yanapata umeme wa Rea ambao ni nafuu kwa wananchi ili maeneo hayo yafunguke Kibiashara kwa watu kujiajiri kwenye shughuli mbalimbali.

Aidha Ummy ameeleza pia umuhimu wa kuboresha Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari ili iwe Rafiki kwa watoto kusoma na hatimae kutimiza ndoto zao pasipo vikwazo”Mimi najua hapa Marungu kuna watoto wana akili sana tukiwaboreshea mazingira ya Shule zao watasoma vizuri na tutapata Madaktari,Wanasheria   kama mimi na hata Marubani Ndugu zangu niamini nitafanya maboresho makubwa kwenye shule zetu .Amesema Ummy Mwalimu”.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...