Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita Chama cha Demkrasia Makini amesema endapo atapata ridhaa ya kuwa Rais na kuongoza serikali.Chama hicho kitafanya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano watanzani ya mwaka 1977 na kuunda katiba mpya itakayo beba matatizo na kero za watanzania.
Mgombea huyo ameyasema mkoani Njombe wakati akifanya kampeni katika eneo la stendi ya zamani ya mji wa Njombe huku akiunga mkono katiba pendekezwa ya Jaji Warioba.
"Ninawaahidi katika serikali yangu ninaenda kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,Ninachukua katiba pendekezwa ya Jaji Warioba,tunarudi kwa wananchi kuchukua maoni yenu na kurekebisha katiba mpya"Alisema Cecilia Mmanga mgombea Urais JMT kupitia chama Cha demokrasia Makini
Amewataka pia kuendelea kuulinda Muungano pamoja na amani ya Tanzania "Tusisahau kuulinda Muungano,kwenye mitandao ya kijamii kuna wajinga wachache wanatuma ujumbe eti tarehe 28 endapo Chama X hakitaingia madarakani,wananchi tuandamane na kuingia barabarani ninawahusia tusiingie barabarani tutapoteza amani yetu"amesema Cecilia Mmanga
Vile vile ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kupiga kura ili kupata viongozi watakao kuwa sahihi kuongoza taifa"Ninawaomba ndugu zangu tarehe 28 mjitokeze kwa wingi kupiga kura na pia ninwahusia msiende makundi kwenye kupiga kura,kama ulienda kujiandikisha ukiwa mmoja mmoja na kupiga kura nendeni mmoja mmoja"amesema Cecilia Mmanga
Hata hivyo amesema serikali yake itakwenda kukuza na kujenga kiswahili ili kutanua wigo wa lugha hiyo kimataifa"Ndani ya serikali yangu ninawaahidi endapo mtu atabeza kiswahili na kudharau kishwahili huyo hatufai katika taifa hili la Tanzania"Cecilia Mmanga mgombea Urais JMT kupitia chama Cha deomkrasia Makini
Wakati mgombea wa Chama hicho akiwa mkoani Njombe,Naye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mapema leo Oktoba 14,2020 amewasili Ukerewe kuendelea na kampeni za Chama chake.
Kwa upande wa mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt,John Pombe Magufuli yeye ameendelea na kampeni zake jijini Dar Es Salaam huku leo akiwa katika jimbo la kawe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...