*Asema ukiona mtu anazungumzia uvunjifu wa amani, huyo ameshindwa uchaguzi
*Aweka wazi akitoa wa kuwambia wafanye vurugu, wamjibu aende yeye,mkewe
Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Bagamoyo
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amewaambia Watanzania wasikubali kuvuruga amani ya nchi kwasababu tu ya kurubuniwa na watu wasioiakia mema nchi yetu na kwamba mtu akisema siku ya uchaguzi vijana waende barabarani wamwambie aende yeye na mkewe.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati akiomba ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano, Dk.Magufuli pamoja na mambo mengine Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa Watanzania kuendelea kutunza amani iliyopo na wasikubali kwa namna yoyote ile kuivuruga kwani baada ya hapo nchi haitakuwa salama na hakuna litakalofanyika.
Tanzania tunataka amani hata baada ya uchaguzi huu, nchi ikiharibika wanaopata shida ni akina mama , watoto, wazee.Wewe kijana ukiamua kwenda kufanya fujo huna babu, bibi, baba, mama, mdogo wako,Unaangaliaje maisha yao?Tumekuwa na chaguzi huko nyuma na huu utapita , ukiona mtu anazungumzia uvunjifu wa amani ujue huyo ameshashindwa uchaguzi, amani ni muhimu sana, amani ikikosena hata barabara za lami hazitajengwa, tuilinde ndugu zangu hii amani.
"Naipenda hii nchi, nataka kumaliza nikiacha nchi ikiwa na amani kwa hiyo msikilize watu wanaohubiri ugomvi, Tanzania ni tajiri na kuna watu wanaona wivu, nimetoa mfano ukienda kwenye mzinga wa asali hujali nyuki waliotengeneza asali bali utakwenda na moshi na moto ili kuua wale nyuki, wanaozungumzia uvunjifu wa amani wanataka kuchukua madini, hadhabu na rasilimali zetu,"amesema Dk.Magufuli.
Pia amesema kuna mgombea mmoja anaseme wakichaguliwa kushika nchi, madini yote, misitu yote na rasilimali za nchi hii wataweka rehani.Madini na rasilimali nyingine tulizonazo ndizo zinatumika kujenga barabara , kulipa ada."Rasilimali inayotoa fedha kwa ajili ya wazee na watoto kupata huduma za afya bure unaiweka rehani?
"Ni kama vile kuiweka nchini kwenye utumwa, ninayosema hapa kuna siku mtanikumbuka.Watu waliokuwa nje ya nchi hatujui wameweka mikataba gani kwa ajili ya wananchi.Watu hao ambani ni vibara muwakatae kwa kuwanyima kura siku ya uchaguzi mkuu,"amesema Dk.Magufuli.
Wakati huo huo amesema uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu, ni uchaguzi utakaoamua kupata viongozi ambao watalinda uhuru wa nchi au kupata viongozi watakavuruga muungano, ni uchaguzi ambao utaamua kupata viongozi wazalendo kwa nchi yao au kupata viongozi vibaraka wa makuadi.
"Uchaguzi huu utaamua kupatikana kwa viongozi wa kulinda amani yetu au viongozi wa kuvuruga, utaamua kama tuendelee na umoja na mshikamano au kutugawana, uchaguzi utaamua tuendelee kulinda rasilimali zetu au kuchagua viongozi watakaoweka rasilimali zetu rehani.Uchaguzi utaamua kupata viongozi wa kulinda tamaduni na desturi zetu au kupata viongozi watakaoleta tamaduni za nje ambazo kwetu hazikubaliki. "Mkinichagua mimi na wenzangu tutahakikisha mapinduzi matukufu yanalindwa,"amesema Dk.Magufuli.
Amesisitiza amefika kwao kuwaomba kura, amekwenda kwa heshima,amefurahi na zaidi ni baada ya kufika katika mkutano na kumkuta Rais mstaafu Jakaya Kikwete naye yuko hapo."Watangulizi wangu kuanzia Baba wa Taifa , Julius Nyerere wameongoza nchi yetu vizuri, baada ya Nyerere alikuja mzee Mwinyi, akamuachia Mzee Mkapa na kisha akamuachia mzee Kikwete na sasa mimi.
"Nipeni na mimi miaka mingine mitano ili niwe nimeongoza kwa miaka 10 kama walionitangulia.Nawapenda sana ninawapenda sana Bagamoyo, nawapenda sana Pwani, mim ni mtoto wenu, nawaomba amani tumeitunze wakati wote, lazima tuilinde, tusije kukadanganywa na mtu yoyote iwe kwa kupewa fedha au viroba tusikubali kudanganywa,"amesema Dk.Magufuli.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...