*************************************

Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu leo amekutana na Mzee Mshenga Yusuf ambae hivi karibuni ilionekana video yake akimuombea kura Ummy na Mgombea Urais Dk John Magufuli.

Mzee Mshenga mwenye umri wa miaka 120 ,amemueleza Ummy Mwalimu kuwa amefurahi kuitikia wito wake”Nilikuwa nikidhani Odo ni Jitu kubwa kumbe ni mtu wa kawaida na Muungwana ,Nimefurahi umekuja kuniona mwanangu mimi nakuombea heri wewe na Magufuli tena mwambie Mhe Magufuli yeye atapita tu maana amefanya makubwa”Amesema Mzee Mshenga Yusuf.

Kwaupande wake Ummy ameeleza kupokea ombi la Mzee Mshenga la kutaka kuwekewa umeme na kusema atalitekeleza na amemshukuru kwa Uzalendo wake kwa Nchi yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...