Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ndani ya siku 100 atajenga matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Msingi Mapambano iliyopo kata ya Magaoni.
Mgombea Ubunge Ummy amesema”Endapo mtanichagua wana Magaoni nitahakikisha Mshahara wangu wa kwanza wa Mwezi Novemba nautumia kwa ajili ya Ujenzi wa matundu ya Vyoo 12 kwa ajili ya Shule ya Msingi Mapambano, ili watoto wetu hususani wakike waweze kupata sehemu nzuri ya kujistiri pindi wanaposhikwa na haja”Amesema Ummy Mwalimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...