Na Samwel Mtuwa - Lindi

MKUU wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi leo ameipongeza na kuishukuru  Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kutoa  mrejesho wa utafiti wa awali unaoonesha uwepo wa Madini mbalimbali Wilayani Liwale Mkoani Lindi.

Akizumgumza mapema baada ya kumalizika kwa Uwasilishwaji huo Zambi amesema mrejesho huu utasaidia kufahamu juu ya rasilimali Madini zinazopatikana mkoani Lindi ikiwa pamoja na kuongeza fursa za Uwekezaji katika sekta ya Madini.

"Ukweli ni kwamba sekta ya Madini ina mchango mkubwa katika pato la taifa na sisi hapa Lindi tunapopata taarifa Kama hizi tunasikia faraja Sana,  nawashukuru sana wataalam kutoka GST"amesema  Zambi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Rehema Madenge ameiomba GST kuwasilisha taarifa za Madini katika Wilaya nyingine za Mkoa wa Lindi  zinazobainisha uwepo wa Madini.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale  Mbwana Kambangwa amesema kuwa utafiti huo wa awali utafungua milango ya uwekezaji katika sekta ya Madini ndani ya Wilaya ya Liwale.

Uwasilishwa wa mrejesho wa Utafiti awali imewakutanisha  na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Katibu Tawala Mkoa wa Lindi , wakuu wa vyombo vya ulinzi na usala ma mkoani Lindi , Kamanda wa TAKUKURU mkoani Lindi,  watumishi mbalimbali  kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...