…………………………………………………………………………………….
 
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amekamilisha haki yake ya kikatiba kwa kupiga kura katika eneo la Kilimani, jijini Dodoma.
Katika eneo hilo ambapo pia awali na baadaye walionekana viongozi wengine mbalimbali wa Serikali, Chama na taasisi binafsi, Dkt. Abbasi alikaa kwenye foleni kama kawaida na wananchi wengine na alipomaliza kupiga kura akasisitiza:
 
“Nimekamilisha haki yangu ya kikatiba kwa furaha sana kwa sababu tukiwa pale kwenye foleni tunapiga stori za hapa na pale wananchi walikuwa wanasema sio wote tuliopiga nao kura mwaka 2015 leo wamepata bahati tena kama hii kwa maana ya uhai kushiriki nasi. Hivyo ni jambo si tu la kikatiba lakini lenye hisia kubwa kibinadamu na kiroho mtu anapolitimiza.”
Dkt. Abbasi alieleza kuridhishwa na hali ya utulivu kituoni hapo na kusisitiza ambao hawajakamilisha haki yao wajitokeze kuwahi kabla ya muda uliowekwa na Tume kukamilika.
 

“Kituoni kwetu hapa na kwingine nilikopita hapa Dodoma hali ni shwari. Tume imejipanga hasa utaratibu ni mzuri na wa uhakika kwani kila hatua unaelekezwa wasimamizi na makarani wa uchaguzi na mawakala wa vyama wanajiridhisha kwa kila jina linalotajwa.
 
“Ukiacha kelele za baadhi ya wanasiasa wachache Watanzania wengi wameitikia wito wa amani na wengi tuliopiga nao kura hapa kila mmoja anasema anarejea nyumbani au kwenye shughuli zake kwa ajili ya kuendelea na masuala mengine atasubiri matokeo kuanzia jioni,” alisema Dkt. Abbasi.
 
Dkt. Abbasi ametumia muda huo pia kuvipongeza vyombo vya habari kwa kazi kubwa waliyoifanya kuripoti kampeni za vyama mbalimbali na kuvitaka kumaliza vyema zoezi hili la uchaguzi kwa kufuata taratibu za Tume hasa katika kutangaza matokeo ya awali hadi yale ya mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...