Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, Mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Masasi, Geofrey Mwambe (kulia) na mgombea Udiwani wa CCM katika Kata ya Mkomaindo, Masasi,Shaibu Kayembe katika mkutano wa kampeni aliouhutubia kwenye uwanja wa CCM Sabasaba


Wananchi wa Masasi wakimshangilia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa kampeni katika uwanja wa CCM Sabasaba, Masasi


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe, Anna Abdallah baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa CCM Sabasaba, Oktoba 21, 2020.

………………………………………………………………………………………….

*Mama Anna Abdallah amtolea uvivu mgombea anayeshabikia ushoga

WAGOMBEA UBUNGE wawili wa Mkoa wa Mtwara waliotoka vyama vya upinzani na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) wameeleza machungu waliyokuwa wakikumbana nayo wakati wakitaka kuwatumikia wananchi wao.

Wabunge hao Bw. Cecil Mwambe (Ndanda) na Bw. Katani Ahmed Katani (Tandahimba) ambao wamehamia CCM kwenye kinyang’anyiro hiki cha ubunge, wamewaonya wakazi wa Masasi wasifanye makosa ya kuchagua wagombea wa upinzani kwani wataendelea kukosa maendeleo.

Wametoa wito huo jana (Jumatano, Oktoba 21, 2020) kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea ubunge na udiwani wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba kata ya Mkuti, wilayani Masasi, mkoani Mtwara ambako Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi

Bw. Mwambe anayegombea Ndanda na ambaye alihamia CCM akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema licha ya kuwa alikuwa akitamani wananchi wake wapate huduma muhimu kama maji, afya na barabara, haikuwa rahisi kwake kuchangia bajeti ya maendeleo kwa sababu walikuwa wanakatazwa.

“Mambo yaliyokuwa yanafanyika huku Masasi hata sisi kule Ndanda tulikuwa tunayatamani. Hii ni kwa sababu hakuna cha maana kule kilichoandikwa kwa ajili yenu, na mimi ni shahidi. Katika miaka mitano ya ubunge wangu, sijawahi kuitikia NDIYO na madhara yake nimeyaona. Ninawaomba sana, msifanye makosa hayo,” alisema.

Naye Bw. Katani anayegombea Tandahimba na ambaye alihamia CCM akitokea Chama cha Wananchi (CUF), aliwataka wananchi hao wasifanye makosa kwa sababu kule alikokuwa hawana ilani.

“Kama Katani anayeongea hapa mbele yenu, alikuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa na kaikimbia CUF, wewe ni nani mwananchi wa Masasi hata upinge maendeleo ya nchi hii? Tena niwaambie, kule hakuna ilani. Nawaomba wana Masasi msifanye makosa ya kuchagua wagombea wa upinzani, sisi wenzenu tumeyaona tukiwa Bungeni.”

“Ukienda Bungeni kutaka kusema Masasi tuna shida ya umeme, wakubwa wanasema kapinge bajeti. Tutaupataje umeme? Tumekwenda Bungeni tumepiga plasta, sasa ukitaka kuomba umeme, utaongea vipi na wewe midomo umeifunga plasta?”

“Wana Masasi msitucheleweshe, hii gari ya Dkt. Magufuli inatelemka kwa kasi kuleta maendeleo huku mikoa ya Kusini. Acheni Geofrey Mwambe awe mbunge wa jimbo la Masasi, alete maendeleo,” alisisitiza.

Wakati huohuo, mwanasiasa mkongwe na Waziri Mstaafu, Mama Anna Abdallah alisema anashangazwa na tabia ya mgombea urais ambaye anatangaza kwamba ndoa za jinsia moja ni haki ya msingi ya wananchi.

“Yuko mgombea wa urais ambaye yeye anasema haonei aibu ushoga eti anauunga mkono. Yaani mwanaume amuoe mwanaume mwenzake na mwanamke amuoe mwanamke mwenzake.”

“Anasema eti ni haki za binadamu. Hivi kama baba yake angemuoa mwanaume mwenzake au mama yake angeolewa na mwanamke mwenzake, yeye leo angekuwepo na angekuja kugombea urais?”

“Rais wa namna hiyo ana mawazo ya kishetani, hakuna dini hata moja inayosema juu ya ushoga. Hata wanaogombea kwa kupitia chama hicho ninaanza kuwatilia shaka. Hakuna ushoga katika nchi hii, hatutakiii! Haiwezekani, sisi tulioko hapa tumezaliwa na sisi tumezaa. Watoto wetu waache kuzaa kwa ajili ya mtu mmoja anayesema hiyo ndiyo haki. Hakuna haki kwenye ushoga, ni dhambi,” alisisitiza.

Mapema, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Masasi, Bw. Rashid Chuachua alisema katika wilaya hiyo, ndani ya miaka mitano, waliwezaa kujenga madarasa 108 ya shule za sekondari na mengine 355 ya shule za misngi.

Alisema kiasi cha sh. bilioni 3.5 kilitolewa kwa ajili ya elimumsingi bila malipo huku sekta ya afya ikiboreshwa kwa kujenga kituo cha afya cha Mbonde kwa gharama ya sh. milioni 500 na hospitali ya Mkomaindo ikipatiwa jengo la upasuaji lililogharimu sh. milioni 228.

“Mradi wa maji unaendelea kujengwa na ukikamilika, hatutakuwa na shida kabisa ya maji hapa Masasi,” alisema na kuwaombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Masasi, Bw. Geofrey Mwambe; na wagombea udiwani 14 wa CCM wa jimbo la Masasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...