Yassir Simba,Michuzi Tv 


Mzunguko wa tano wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara VPL umeendelea leo tarehe 03 October, 2020 kwa michezo tofauti kupigwa huku katika dimba la Mkapa jijini Dar Es Salaam Yanga wakiwakaribisha Coastal Union Wagosi Wakaya Kutoka Mkoani Tanga.


Mchezo huo uliopigwa majira saa 1:00 usiku ulishuhudia wananchi timu ya Yanga wakipiga mpira mwingi yani pira biriani pira Mandi, dakika 45 za kipindi cha kwanza ziliisha suluhu kwa timu zote kufungana huku Yanga wakihitaji sana matokeo katika kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ya Yanga wakiwaingiza Deus Kaseke pamoja na Haruna Niyonzima wakichukua nafasi za Zawadi Mauya na Shomary Kibwana, ilikuwa ni dakika 48 ya mchezo mpira wa krosi uliopigwa na Deus Kaseke ukawekwa wavuni na Carlos Carlinhos huku dakika 52 Haruna Niyonzima akawela bao la pili huku Yacouba Sogne akahitimisha ushindi mnono wa mabao 3 -0 kwa Yanga dhidi ya Coastal Union. 


Mara baada ya matokeo hayo Yanga imesogea kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 13 mara baada ya kucheza michezo mitano huku Coastal Union wakishika nafasi ya 16 wakiwa na alama 4 wakicheza michezo 5.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...