Na Jusline Marco-Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira amewataka wanawake wajasiliamali nchini kuthamini na kutumia bidhaa wanazozitengeneza ili kuwa mfano kwa wengine na kuweza kukuza biashara zao zitakazo kidhi soko la kimataifa.
Akifungua kongamano la kwanza la wanawake wajasiriamali jijini Arusha likiwa na lengo la kumuinua mwanamke kiuchumi Mhe.Mgwira amesema kuwa katika kuendelea kuzitangaza bidhaa husika lazima kuwe na uwezo wa kulifikia soko ambalo linajitokeza na kuziuza bidhaa hizo.
Amesema kuwa ili bidhaa iweze kuwa na kibali katika jamii inayowazuka ni vyema mtengenezaji wa bidhaa husika akaithamini bidhaa yake kwa kuitumia yeye binafsi ili kuweza kuthibitisha kuwa kile anachokifanya kina ubora na viwango vinavyohitajika.
Awali akizingumza katika kongamano hilo mkurugenzi mkuu wa kampuni ya I AM WOMAN PRENEUR LIMITEDS,Miss Gladness Katenga amesema kuwa lengo kubwa ni kusaidia mwanamke wa kitanzania kujua namna ya kukuza biashara ili kuweza kulifikia soko.
Aidha amesema kuwa katika kongamano hilo ambalo lomekutanisha wanawake wajasiriamali wanaopenda kujifunza ujasiriamali kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kumsaidia mwanamke wa kiafrika ajue ni kwa jinsi gani anaweza akakuza biashara yake ili iweze kuwafikia watumiaji ndani na nje ya nchi.
"Sisi wanawake tunauwezo wa kuungana na kujengana kifikra na hata kiuchumi kwani kujijenga kwa mwanamke kunatokana na kukuza mtandao wake".Alisema Gladness
Ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa mwanaume,kongamano hilo pia limeshirikisha wanaume kwani changamoto nyingi ambazo mwanamke hupitia wanaume wengi huwa hawazifahamu hivyo kama taasisi wanaamini kujijenga kwa mwanamke kunatokana na mwanaume jasiri nyuma yake ambapo katika kukua pamoja kunapelekea uwepo wa kikazi chenye kujituma katika kufanya kazi.
Naye mmoja wa washiriki katika kongamano hilo Injinia Wardaesta Mashimark ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Giadi Consultance amewataka wanawake wenzake kujishughulisha katika shughuli mbalimbali ambapo amesema kuwa ulemavu siyo sababu ya kutokufanya kazi ambazo mtu amekusudia kuzifanya.
Ameeleza kuwa ni vizuri kila mwanamke akatoka na kujishughulisha kwa kufanya biashara ndogondogo ambazo zinaweza kukuingizia kipato ambacho ukikitumia vyema wanauwezo wa kuanzisha biashara kubwa.
"Mwanamke anamchango mkubwa katika jamii hivyo ni vyema akawajibika katika shughuli mbalimbali kusudi kuweza kuleta urahisi katika familia kwa kusaidiana majukumu kwami mwanamke yeyote ni mkuu hivyo anapaswa kudhihirisha ukuu huo kwa kufanya kazi."Alisema Injinia Wardaesta
Vilevile ametoa wito kwa wanawake hususani walio na ulevu wa viungo kutojibweteka na kuwa tegemezi kwa kisingizio cha ulemavu bali wanapaswa kutambua kuwa ulemavu wa viungo usiwe sababu ya kutokufanya kile ambacho unakusudia kukifanya kusudi kuweza kutimiza ndoto zao kwa kutimiza mahitaji yao naya familia kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira akifungua kongamano la kwanza la wanawake wajasiriamali liliandaliwa na kampuni ya I AM WOMAN PRENEUR ya nchini Uingereza lililofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa kampuni ya THE RADICAL LEAP iliyopo nchini Uingereza,Noreen Makosewe akizungumza na wanawake wajasiriamali jijini Arusha katika Kongamano la wanawake.
Baadhi ya wanawake washiriki wa kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali ikiwemo,Kenya,Afrika kusini pamoja na Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji wa kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...