Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Magese Bulayi akisoma lisala kwa niaba ya Katibu Mkuu Uvuvi- Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Rashid Samatamah wakati wa kikao kilichoshirikisha wadau mbalimbali wa uvuvi wakijadili aina ya vifaa vya meli itakayotengenezwa na Serikali ya Japan.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
 SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuboresha ukuaji wa sekta ya Uvuvi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya Uvuvi ili kuweza kuongeza mapato ya serikali yatokanayo katika sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Magese Bulayi  akimwakilisha Katibu Mkuu-Uvuvi, wizara ya Mifugo na Uvuvi, Rashid Tamatamah, wakati kufungua kikao wa Uvuvi kilichofanyika leo Oktoba Mosi, 2020 jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa serikali inatambua umhimu wa uwepo wa Shirika la Uvuvi la Tanzania (Tanzania Fisheries Corporation-TAFICO) kwani inachangia maendeleo ya Sekta ya Uvuvi na inachangia katika uchumi wa nchi.

Amesema kuwa katika kuhakikisha Shirika la Uvuvi la Tanzania (Tanzania Fisheries Corporation-TAFICO) linahitaji mikakati mipya ya uendeshaji na kiutendaji ikiwemo kufufua shirika hilo.

Hata hivyo Serikali ya Japan imetoa msaada wa Yen Milioni 200 ambazo ni takribani ya shilingi za kitanzania Bilioni 4.2 kupitia programu ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii kwaajili ya kununua vifaa vya uvuvi vitakavyosaidia katika kuboresha sekta ya uvuvi hapa nchini.

"Mnamo Disemba, 27, 2019 Serikali ya Tanzania ilitiliana sahihi na Serikali ha Japani Mkataba wa Utekelezaji wa Program uchumi na Maendeleo ya Jamii ( Economic and Social Development Programme(ESDP)),ili kuipa TAFICO vifaa vya Uvuvi na aasa taratibu za manunuzi ya vifaa zimeanza." Amesema Bulayi.

Licha ya hilo Bulayi amesema kuwa vifaa vitakavyonunuliwa kupitia Program uchumi na Maendeleo ya Jamii ni pamoja na meli moja ya Uvuvi, Ice Plant na Cold Storage Facility ambavyo serikali ya Japan itanunua, itasafirisha, itafundisha juu ya matumizi ya mitambo na inasimika mitambo hiyo katika eneo la Ras ya Mkwavi.

Hata hivyo katika Kikao hicho cha wadau wa Uvuvi watajadili msimamo wa aina ya vifaa vinavyohitajika kabla ya Manunuzi ya Vifaa hivyo ili kuwasilishwa kwa mtengenezaji wa meli.

Amesema maazimio ya kikao hicho ndio yanayohitajika ili mtengenezaji wa Meli aweze kutengeneza kulingana na eneo linalokusudiwa kulingana na vigezo vitakavyowesha kupatikana kwa vifaa vya TAFICO vitakavyonunuliwa kupitia ufadhili wa Japan.

Ukweli ni kwamba nchi yetu imebarikiwa kuwa na Bahari, Maziwa, Mabwawa na Mito yenye rasilimali nyingi za Uvuvi ambazo zimegawanyiko kulingana na mifumo ya Ikolojia ambapo kazi kubwa ya Shirika la Uvuvi la Tanzania (Tanzania Fisheries Corporation-TAFICO) ni kuendeleza Uvuvi hususan katika Ukanda wa uchumi wa Bahari Kuu na maji kitaifa.

"Rasilimali za uvuvi bado hazijachangia kikamilifu katika pato la taifa na endapo Sekta ya Uvuvi ikikua inawezesha kuongeza mapato ya fedha za kigeni kutokana na kusafirisha nchi ya nje mazao ya uvuvi, kuongeza ajira na kupunguza Uvuvi haramu." Amesema Bulayi

Kikao cha wadau wa Uvuvi kimeshirikisha wadau kutoka Sekta binafsi zenye uzoefu, kampuni za Uvuvi, TDDB, THA, DMI, TAFIRI, TASAC, Menejimenti ya Shirika la Uvuvi la Tanzania (Tanzania Fisheries Corporation-TAFICO), Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na waaakilishi wa Idara ya Uvuvi.

Baadhi ya wadau wa Uvuvi wakichangia mada katika kikao cha kujadili aina za vifaa vya Shirika la Uvuvi la Tanzania (Tanzania Fisheries Corporation-TAFICO)  kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Uvuvi wakimsikiliza muwasilisha mada leo katika kikao cha kujadili aina za vifaa vya Shirika la Uvuvi la Tanzania (Tanzania Fisheries Corporation-TAFICO)  kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...