Na Jane Edward Arusha, Michuzi TV

Taasisi ya wanawake wahasibu nchini ( tawca) imesema moja ya malengo yao  makuu nikuhakikisha taaluma ya uhasibu inaheshimika katika nyanja zote ili kuweza kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake nakuendana na ushindani wa teknolojia.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo la tatu la wahasibu wanawake lililoshirikisha zaidi ya wanawake miatatu,mwenyekiti wa taasisi hiyo Dr.Neema Kiure amesema kua lengo la kongamano hilo nikuwakutanisha wahasibu wanawake katika kujadili mafanikio na changamoto zinazo mkumba mwanamke katika masuala ya uongozi

‘’Kukutana kwetu leo kunalenga kujadili masuala ya wanawake hasa katika  uongozi lakini pia kuwawakilisha wanawake wengine ambao hawajapata fursa ya kuja katika kongamano hilo ,ukizingatia katika kipindi hiki ambacho teknolojia inakuwa kwa kasi ‘’Alisema Dr Neema Kiure

Balozi Liberata Mulamula ambaye pia ni muhadhiri chuo kikuu cha George Washington Marekani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo amesema kuwa katika wakati huu ambao Taifa linaelekea katika uchaguzi ni vyema jamii ikatambua kuwa wanawake wanaweza katika nafasi za uongozi na kupeperusha bendera ya Tanzania

‘’Mamlaka za juu katika kipindi hiki zitambue utendaji kazi wa wanawake  na kujipanga  kutatua changamoto na kuondoa mfumo dume katika baadhi ya maeneo yanayoongozwa na wanawake’’Alisema Balozi Liberata Mulamula

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa kongamano la Wahasibu wanawake akiwemo Afisa mkuu wa fedha shirika la umeme Tanzania Tanesco Bi Renata Ndege alisema lengo la kongamano ni kuwajenga wanawake nafasi za uongozi na wao kama tanesco wamekuwa mfano wa utendaji kazi kwa kuwapa fursa wanawake kuongoza nafasi mbalimbali.

 Ndege Ameongeza kuwa shirika la umeme nchini limefanikiwa kutoa huduma kwa wananchi kutokana na kuwa na viongozi wanawake mahiri wa ngazi za juu wenye uwezo wa kusimamia masuala ya fedha

Kongamano hilo la tatu la wanawake Wahasibu [TAWCA]  ambalo limewakutanisha wanawake kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania inatajwa kuwa suluhisho la utatuzi wa changamoto za uongozi zinazowakabili wanawake hao hasa katika suala la mfumo dume.

 Renata Ndege, Afisa Mkuu wa fedha Shirika la umeme Tanesco akizungumza na waandishi wa Habari katika kongamano la wanawake wahasibu (Picha na Jane Edward Arusha)

 

 Balozi Lebarata Mulamula akifungua Mkutano wa washiriki wa kongamano la wanawake wahasibu Mkoani Arusha(Picha na Jane Edward, Arusha)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...