


Na Agness Francis, Michuzi tv
SHIRIKA la utu wa mtoto CDF limeandaa ghafla ya ya maadhimisho siku ya mtoto wa kike ambapo mgeni rasmi alikuwa ni katibu mkuu-wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, John Jingu ambapo amesisitiza umuhimu wa kumlinda mtoto wa kike.
Hayo ameyasema Katibu mkuu-Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, wazee na watoto, John Jingu wakati wa hafla hiyo ya maaadhimisho ya siku ya mtoto wa kike wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wanaopinga ukatili dhidi ya mtoto wa kike ambapo kitaifa yamefanyika Jijini Dar es Salaam, Amesema kuwa ipo haja ya kutokomeza ukatili wa kijinsia hasa mashuleni.
"Kwa kukabiliana na hili serikali imeanzisha madawati 155 ya kupinga ukatili wa watoto mashuleni, Ambapo watoto watapata fursa ya kuelezea kwa uhuru kabisa, na walimu wamepewa pia mbinu za kushughulikia changamoto ambazo zinawakabili watoto hao wa kike." Amesema Jingu.
Aidha Mkurugenzi wa shirika la jukwaa la utu wa mtoto CDF, Koshuma Mtengeti ameeleza kuwa ipo haja ya kuwasaidia watoto hao wanaokumbwa na changamoto ya mimba za utotoni ikiwa asilimia ishirini na saba kati ya mia hupata ujauzito mashuleni wakiwa na umri chini ya mika 18.
Vile vile Mwanafunzi wa shule ya sekondari Kitunda, Pili Athumani amesema kuwa sheria iliyowekwa na serikali ya kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia itamsaidia mtoto huyo katika kutimiza malengo yake ya hapo baadae.
"Mtoto wa kike atakapoelimishwa sasa na kulindwa dhidi ya madhila hayo ndiye atakayeweza kujenga taifa la kesho." Amesema Pili Athuman.
Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji haki elimu John Kalage amemalizia kwa kusema kuwa ili kuondokana na vikwazo hivyo vinavyomsababishia mtoto wa kike kutopata elimu , Ni kujenga usawa wa kijinsia katika uelimishaji wa watoto.
"Sio watoto wote wa kike wanapata nafasi ya kumaliza elimu ya juu pindi wanapoanza kidato cha 1 wengi wao huishia njiani."Amesema Mkurugenzi mtendaji hakielimu Kalage.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...