Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akitoa maneno ya utangulizi
wakati wa sherehe fupi za kukabidhi Hati za Hakimiliki za kimila.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Tito
Luchagula akisoma leo taarifa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika
sherehe fupi za kukabidhi hati za Hakimiliki za Kimila kwa vijiji
vya Ukondamoyo, Mole na Usanganya.
Baadhi
ya wakazi wa Kijiji cha Ukondamoyo wilayani Sikonge wakiwa katika
sherehe fupi leo ya kukabidhi hati za Hakimiliki za Kimila kwa vijiji
vya Ukondamoyo, Mole na Usanganya.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri akitoa hotuba leo wakati
sherehe fupi za kukabidhi hati ya hakimiliki ya kimila za awamu ya pili
224 kwa wanavijiji vya Vijiji vitatu na hivyo kufikisha Hati 856 ambazo
zimekwishatolewa chini Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania(MKURABITA).
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri( kushoto) akisalimiana na Meneja
wa Urasimishaji Ardhi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara
za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Antony Temu(kulia) wakati apowasili leo
katika Kijiji cha Ukondamoyo kwa ajili ya kukabidhi Hati za Hakimiliki
za kilima.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge
Peres Magiri (kulia) akimkabidhi leo hati ya hakimiliki ya kimila mmoja
wa wakazi wa Kijiji cha Ukondamoyo Johari Selemani(kushoto) baada ya
maeneo yake kuhakikiwa na kupimwa chini ya Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).Mkuu
wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri(mwenye suti nyeusi) akiwa katika
picha ya pamoja na wakazi wa Kijiji cha Ukondamoyo ambao maeneo yao
yalihakikiwa na kupimwa na kukabidhi hati ya hakimiliki ya kimila chini
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania(MKURABITA).
Picha na Tiganya Vincent
********************************
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge imetakiwa kuhakiki na kupima mashamba ya wanavijiji ambayo hayajapimwa ili waweze kupatiwa hati ya hakimiliki ya kimila kwa ajili ya kuyaongezea thamani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri wakati akikabidhi hati ya hakimiliki ya kimila za awamu ya pili 224 kwa Vijiji vitatu na hivyo kufikisha Hati 856 ambazo zimekwishatolewa chini Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA).
Alisema hatua hiyo itasaidia kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao utasaidia kuondoa migogoro miongoni mwa wanavijiji wao kwa wao.
Magiri alisema kuwa Wilaya ya Sikonge ina Vijiji 71 lakini ambavyo wakazi wamepimiwa maeneo yao ni 12 na kubaki 59, jambo ambalo linahitaji kufanyia kazi ili kukamilisha vyote.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatatua tatizo la mwingiliano wa maeneo 102 katika Vijiji vya Ukondamoyo, Mole na Usanganya ambalo ulisababisha MKURABITA washindwe kuandaa hati za Hakimiliki za Kimila kwa wananchi.
Alisema sanjari na hilo ni vema wanakijiji 797 ambao hawakujitokeza wakati MKURABITA wakihakiki maeneo katika vijiji vyao wajitokeza ili nao waweze kupimiwa maeneo yao kwa ajili ya kupatiwa hati.
Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe aliwataka wanavijiji kuhakikisha wanatumia Hati ya Hakimiliki za Kimila wanazopatiwa kuendesha kilimo na biashara zao kwa tija ili kuchangia katika maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Alisema hati hizo walizopewa ni mtaji ambao wanatakiwa kuutumia kujiongeza kipato kwa kuandaa mipango mizuri ambao itawawezesha kunufaika na fursa ya mikopo katika Taasisi za Fedha.
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) hadi hivi sasa umesharasimisha rasilimali na biashara za wanyonge katika Wilaya 52 kwa upande wa Tanzania bara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...