*TFRA yajivunia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kwa upatikanaji wa Mbolea kwa Wananchi.

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema kuwa matumizi  ya Mbolea imeongezeka pamoja uzalishaji katika msimu wa kilimo wa kutoka Tani 296,036 kwa  2015/2016 hadi kufikia Tani 440,000  kwa 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 48.6.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Stephan Ngailo wakati akitangaza maadhimisho siku ya Mbolea Duniani ambayo hufanyika kila Oktoba 13 ya Mwaka ambayo yatafanyika Dakawa  mkoani Morogoro.

Ngailo amesema kuwa katika Maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Kilimo Japhet Hasunga huku wadau mbalimbali watajumuika ikiwemo maonesho ya Mbolea zinazozalishwa nchini.

Amesema Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni Kuwezesha Wakulima Wadogo kupata Mbolea Bora,Kwa wakati na kwa Bei Nafuu na kuongeza kuwa upatikanaji wa Mbolea Bora ni kuongeza uzalishaji kwa Wakulima na kuongeza mnyororo wa thamani katika mazao.

Ngailo amesema kuwa lengo la Maadhimisho ya siku Mbolea Duniani ni kupata wigo mpana zaidi wa kuelezea masuala mbalimbali katika Tasnia ya Mbolea ikiwemo mafanikio ya Tasnia ya Mbolea nchini.

Aidha amesema Maadhimisho hayo ni muhumu katika kutoa elimu kwa wadau wa Mbolea hususan wakulima na wafanyabiashara wa Mbolea ili waweze kujua mifumo mbalimbali ya utengenezaji wa mbolea ,usambazaji na upatikanaji wa Mbolea nchini pamoja na fursa zilizopo na hali ya uwekzaji katika mnyororo wa thamani wa Mbolea.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli ,TFRA imekuwa na mafanikio mengi  kwa Mamlaka kuendelea kuimarisha kwa mifumo ya Udhibiti na ubora wa Mbolea  ili kuhakikisha kuwa Wakulima wanapata mbolea bora kwa wakati na bei ambayo mkulima anaweza kuimudu na huku Mbolea 103 zikiwa zimesajiliwa katika mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2019/2020.

Aidha amesema katika miaka mitano iliyopita kumekuwa na uongezeko la idadi ya viwanda vyab kuzalisha Mbolea na visaidizi vya  Mbolea nchini vimejengwa vinne kabla ya hapo havikuwepo kabisa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti  wa Mbolea Tanzania (TFRA) Stephan Ngailo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani yatafanyika Dakawa mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...