BALOZI wa China Wang Ke na Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira wakionyesha makubaliano ya ushirikiano baina ya Ubalozi wa China na Agri Thamani
Foundation
Na Patricia Kimelemeta
BALOZI wa China umekubali kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Agri Thamani Foundation kulisaidia shirika hilo katika maeneo ya afya, elimu na kilimo ili kuwawezesha wanawake na mabinti kujitegemea kiuchumi.
Makubaliano hayo yamefanyika Oktoba 14, Mwaka huu ikiwa ni siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni sehemu ya kumuenzi.ambapo Balozi wa China,Wang Ke amesema kuwa ubalozi huo upo tayari kuchangia maendeleo ya jamii kwa kada hiyo ili kuhakikisha wanapiga hatua za kimaendeleo.
Amesema kuwa wanawake na mabinti watakaonufaika na msaada huo ni wale wanaotoka mikoa na vijiji mbalimbali nchini.
Amesema kuwa, katika kuelekea siku ya watoto wa like Duniani inayofanyika Octoba 11 kila mwaka huu Ubalozi umekabidhi msaada wa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi 1500 wa shule za sekondari.
"Leo nimekabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi 1500 wa shule za Sekondari nchini Tanzania ili waweze kujisitiri hasa katika kipindi hiki ambavho baadhi ya wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mitihani" amesema Wang Ke.
Ameongeza kuwa, msaada huo umepokelewa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la upokelewa na Shirika la Agri Thamani,,Neema Lugangira ili kuhakikisha unafika kwa walengwa.
Amesema kuwa taulo hizo zitapelekwa kwenye Mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Tanga, Dodoma na Lindi ambapo watoto hao wa kike wanatoka kwenye familia zenye uhitaji.
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo, Neema Lugangira alimshukuru balozi Hugo kwa utayari wake wa kushirikiana na Shirika la Agri Thamani kwa madai kuwa ushirikiano huo utasaidia kuwainua wanawake kiuchumi pamoja na kuwapatia watoto wakike mahitaji muhimu yakiwamo taulo hizo.
Amesema kuwa, Shirika hilo limekua likitoa elimu ya Lishe kwenye Shule za Sekondari na Masuala ya Hedhi Salama na Afya ya watoto wa kike ikiwa ni sehemu ya Lishe Bora hivyo anaamini kuwa msaada huu wa taulo za kike kwa wanafunzi wa sekondari 1,500 utakuwa msaada mkubwa hususan kwa wale ambao watakuwa kwenye mwaka wa mitihani ikiwemo Kidato cha 2 na cha 4 ambao ndio walengwa.
"Matarajio yangu ni kuhakikisha kuwa msaada huu unafika kwa walenga na ubalozi wa China uendelee kuwasaidia wanawake na watoto wa kike katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii," amesema Lugangira.
Amesema kuwa,mkakati wake ni kuona kuwa wanawapata mahitaji muhimu ambayo yatawasaidia katika shughuli zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...