Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAKUMBUSHO ya Taifa la Tanzania kwa kushirikiana na uongozi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam wameanza mikakati ya kufanya Uwanja wa Taifa kuwa kivutio cha utalii
kupitia maonesho ya kihistoria ya uwanja huo.
Hayo yamedhihirika jana baada ya mkutano kati ya Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuf Singo Omar na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dr Noel Lwoga ambapo katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo la kuanzisha makumbusho ya michezo katika uwanja huo.
Viongozi
hao pia wamejadili kuhusu ushirikiano kwenye uhifadhi na kuendeleza malikale na
urithi wa utamaduni Tanzania ikiwemo Uwanja wa Uhuru uliojengwa kabla ya Uhuru
wa Tanzania (mwaka 1947).
Vile
vile walijadili na kukubaliana juu ya kuandaa maonesho au kuanzisha Makumbusho
ya Historia ya Michezo Tanzania ambayo yanaweza kuwekwa uwanjani hapo.
Mjadala
wao pia ulijikita katika kutumia Uwanja wa Taifa katika kuitangaza Makumbusho
ya Taifa na malikale lukuki zilizopo nchini.
Akizungumza
baada ya mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga
amesema ofisi yake iko tayari kushirikiana na Kurugenzi ya Michezo katika kuvifanya
viwanja vya Taifa kuwa vutivu kwa watalii wa ndani na nje ya nchi na kuwa
sehemu nzuri ya utalii.
“Tumezungumza
vizuri na wenzetu na sisi kama watalaamu wa uhifadhi wa urithi wa asili na
utamaduni tutahakikisha viwanja hivi vinavutia watalii kutembelea kabla na
baada ya mechi zao,” amesema Dkt. Lwoga.
Amesema
jiji la Dar es Salaam lina vivutio vingi vya asili ikiwemo makumbusho, majengo,
fukwe, bustani na uwanja wa Taifa na kwamba inahitajika elimu kwa watu kujua
viko wapi ili waweze kutembelea.
kwa upande wake, Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu Omar amesema ushirikiano na Makumbusho ya
Taifa ni wa muhimu katika kuendeleza malikale nchini ikiwemo Uwanja wa Taifa.
“Sisi
kwa upande wetu tumefurahi sana maana ushirikiano huu umekuja wakati muafaka,”
alisema Omari.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...