Mwenyekiti wa mpito wa Bodi ya Wakurugenzi Vodacom Tanzania PLC, Margaret Ikongo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu wa mwaka (AGM) wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Jacques Marais

======   ======  =======  =======  =======  ====

· Kampuni imerekodi ukuaji wa mapato ya huduma inayoongozwa na data na utendaji wa M-Pesa

· Kampuni inatoa huduma mbalimbali kupitia mtandao unaopendwa zaidi nchini, Vodacom inaendelea kuongoza katika soko la mawasiliano nchini.

30 Oktoba 2020, Dar es salaam: Huduma za Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania Plc zinaendelea kuongeza thamani halisi kwa nchi pamoja na wananchi wake. Mwaka huu kampuni italipa jumla ya Shilingi bilioni 427.5 kama gawio kwa wanahisa wake, ambapo kati ya hizo, Shilingi bilioni 400 ni gawio maalum na Shilingi bilioni 27.5 ni gawio la mwisho wa mwaka wa fedha ulioishia 31 Machi 2020.

Mtandao huu wenye kasi zaidi nchini unajivunia matokeo chanya ambayo umeleta kwa wateja wake na uchumi wa Tanzania kwa jumla ukilinganisha na mwaka wa fedha uliopita. Zaidi ya Shilingi bilioni 327.7 zilitumika kuwalipa watoa huduma wa ndani zaidi ya 120 pamoja na kampuni washirika, huku zaidi ya Shilingi bilioni 1.1 ilielekezwa kwenye uwekezaji wa kijamii nchini, Vodacom ilifunga mwaka wa fedha wa 2019-20 katika hali nzuri. Kampuni pia ilitengeneza ajira zisizo za moja kwa moja kwa Watanzania zaidi ya 135,000 kupitia mawakala, madawati ya huduma kwa wateja pamoja na wafanyakazi huru (Freelancers).

Katika mwaka wa fedha uliopita, Vodacom Tanzania Plc ilirekodi ukuaji wa mapato ya huduma ambayo kwa kiasi kikubwa ilisababishwa na data pamoja na matumizi ya huduma ya M-Pesa. Mapato ya M-Pesa yaliongezeka kwa asilimia 7.4, ikichangia Shilingi bilioni 358.2 kwa jumla ya mapato wakati mapato ya data yalikua kwa asilima 9.8, ikipata jumla ya Shilingi bilioni 180.8.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vodacom leo, Mwenyekiti wa mpito wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom - Bi Margaret Ikongo - alielezea matumaini juu ya utendaji wa kampuni hiyo licha ya huduma kuzuiwa kwa zaidi ya wateja milioni 2.9 kulingana na mahitaji ya usajili wa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha Taifa (NIDA).

"Licha ya mwaka huu kuwa wenye changamoto nyingi katika ushindani mkali wa soko pamoja na mazingira ya udhibiti, kampuni ilirekodi uendeshaji wenye mafanikio ulioletwa na kasi ya kibiashara iliyoanza mwaka wa fedha uliotangulia. Tuliwekeza jumla ya Shilingi bilioni 154.6 katika mtandao wetu pamoja na miundombinu ya Teknolojia ya habari ili kuhakikisha wateja wananufaika na huduma bora na mtandao unaopatikana kote nchini. Matokeo yake ni kwamba tumedumisha mapato ya wateja na uongozi wa hisa katika soko la GSM na matumizi ya pesa kwa kutumia simu za mkononi, na kufikia jumla ya wateja milioni 15.5 wa matumizi ya sauti, data na ujumbe mfupi (sms) na wateja milioni 10.1 wa M-Pesa,” alisema Ikongo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya VodacomTanzania Plc, Bwana Hisham Hendi, alisema kuwa sababu ya matokeo mazuri ya kampuni hiyo ni kufanikisha utekelezaji wa mikakati yake vizuri, ikisaidia kampuni kusogea karibu na maono yake ya kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali na hivyo kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia teknolojia.

"Katika mwaka wa fedha uliopita, matumizi ya data yaliongezeka kwa asilima 14.6, na ukuaji mkubwa ulikuja kutokana na matumizi ya 4G. Hii inaonyesha mahitaji makubwa ya huduma za data kupitia simu za mkononi na pia inathibitisha nia yetu katika kuongeza huduma mbalimbali za data kwa wateja kupitia uwekezaji endelevu katika miundombinu ya mtandao, hii ni pamoja na kuleta simu janja za bei nafuu sokoni lakini pia utoaji wa huduma ya data za bei rahisi, "alisema.

Mbali na kuwekeza katika uboreshaji na upanuzi wa mtandao, Vodacom Tanzania Plc pia ilipanua mfumo wa ikolojia wa M-Pesa kupitia bidhaa na huduma za ubunifu ambazo zilishuhudia ongezeko la wateja pamoja na mgawanyo wa mapato. Wakati huo huo kampuni ilihakikisha wateja wake wanapata matumizi bora na usalama kwenye mtandao.

Hisham alisema kuwa ingawa mazingira ya biashara yanabaki kuwa na ushindani mkubwa, Vodacom Tanzania Plc imejidhatiti katika kutoa huduma bora kwa wateja kupitia ubunifu wa kidijitali pamoja na ujumuishwaji wa kifedha.

"Ubunifu ni kiini cha kila kitu tunachofanya. Tutaendelea kuongoza katika uvumbuzi wa huduma mbalimbali, kuwaleta Watanzania wengi katika uchumi wa jumuishi, kuongeza idadi ya wateja wanaotumia huduma zetu za malipo kupitia simu ya mkononi, kupanua huduma zetu za wateja wakubwa (yakiwamo makampuni) huku tukizingatia ubora na kudumisha mtandao wetu mpana na thabiti zaidi, ” alisema Hisham.

Kuhusiana na athari za ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid19), pamoja na kwamba janga hili lilipunguza matumizi kutoka kwa wateja, Vodacom Tanzania Plc imeweza kuendelea na mipango yake ya kuweka mifumo ya kidijitali nchini.

Katika Mkutano huo Mkuu wa Mwaka, Jaji (Mstaafu) Thomas Mihayo alijiunga na kampuni hiyo iliyoorodheshwa katika soko la hisa la Dar es salaam kama mkurugenzi huru. Wanahisa pia walichagua wakurugenzi mbalimbali wapya pamoja na kuwapitisha wakurugenzi waliokuwepo katika bodi ya kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...